advanced Search
KAGUA
12885
Tarehe ya kuingizwa: 2012/03/10
Summary Maswali
je mwenye saumu anaruhusiwa kukoga janaba?
SWALI
je inafaa mtu kukoga janaba hali akiwa amefunga?
MUKHTASARI WA JAWABU

Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii.

Kukoga janaba kabla ya dhana ya asubuhi:

Kauli ya imam khomeiniy inasema: iwapo mtu atabakia na janaba kwa makusudi hadi wakati wa adhana ya asubuhi ukaingia, au iwapo yeye alikuwa anawajibika kutayamamu lakini akawa hakutayamamu, na akawa amefanya hivyo kwa makusudi, funga yake itabatilika.[1]  Lakini iwapo yeye atakuwemo ndani ya funga nyengine ya wajibu maalumu, kama kama vile funga ya nadhiri, funga yake itakuwa ni sahihi.[2]

Kwa hiyo iwapo mtu atakutwa na janaba ndani ya saumu ya Ramadhani, na tokeo hilo likawa ni kabla ya adhana ya asubuhi, mtu huyo atatakiwa kukoga janaba.

Kukoga janaba baada ya adhana ya asubuhi na kuendelea kipindi kizima cha mchana:

Kauli ya imam Khomeiniy: iwapo mwenye funga ataingiwa na janaba ndani ya mchana (hali akiwa amelala), hakutokuwa na ulazima kukoga papo hapo[3], lakini atawajibika kukoga janaba pale atapotaka kusali adhuhuri, alasiri, magharibi au ishaa. Na wakati wowote ule mtu atakapoamka baada ya adhana ya asubuhi ndani ya mwezi wa Ramadhani, na akajikutia kuwa ana janaba, hata kama atakuwa anajuwa kuwa janaba hilo limempata kabla ya adhana hiyo, funga yake itakuwa ni sahihi.[4]

Kwa hiyo wakati wowote ule mtu akiwemo ndani ya saumu anaweza kukoga janaba.

 


[1] Taudhihul-masaail chenye sherehe ya imam Khomeiniy, juz/1, uk/908-909, suala la 1619. Kauli ya Makaarim Shirazi ni kwamba: ni wajibu kuchukuwa tahadhari ya kuihesabu funga yake kuwa ni batili, lakini iwapo atakuwa hana uwezo wa kukoga au akawa na dhiki ya wakati, anatakiwa kutayamamu, lakini iwapo atakuwa yeye hakufanya hivyo kwa makusudi, basi funga yake itakuwa ni sahihi. Kauli ya Faadhil Lankaraniy: mtu anayetaka kufunga Ramadhani au kulipa funga za Ramadhani, hatakiwi kubakia na janaba kwa makusudi hadi wakati wa adhana ya asubuhi, hivyo basi iwapo yeye atakuwa hakukoga na pia kwa kutokana na dhiki ya wakati akawa hakutamamu, funga yake itabatilika. Kukaa na janaba katika funga nyengine, iwe ni kwa makusudi au si kwa makusudi, huwa hakuleti madhara juu ya funga hizo. Kauli ya Safi Gulpeigaaniy: iwapo mtu atabakia na janaba ndani ya Ramadhani hadi adhana  ya asubuhi bila  ya kukoga, pia akawa hakutayamamu, lakini akawa hakuwa na makusudio ya kufanya hivyo, bali labda  kulikuwa kuna mtu aliyemzuia kufanya hivyo, funga yake itakuwa ni sahihi.

[2] Rejea kitabu kilichopita, uk/909, suala la 1620. Kauli ya Khui na Tabriziy: iwapo yeye atakuwemo ndani ya saumu isiyokuwa ya Ramadhani au katika kuilipa funga ya Ramadhani, bali akawa katika saumu nyengine yenye kumuwajibikia yeye katika siku maalumu, kama vile funga ya nadhiri, funga yake inaonekana kuwa ni sahihi.

[3] Rejea kitabu kilichopita, uk/915, suala la 1632. Kauli ya Faadhil Lnkaraniy: ingawaje inapendekezwa mtu kuchukuwa tahadhari ya kukoga papo hapo. Kauli ya Makarim Shirazi: ni vizuri wakati wowote ule mwenye saumu anapopatwa na janaba kukoga papo hapo, lakini iwapo yeye  atakuwa hakukoga papo kwa hapo, funga yake haitobatilika.

[4] Rejea kitabu kilichopita, suala la1633. Kauli ya Makarim Shirazi: funga yake ni sahihi, iwe anajuwa kuwa amepatwa na janaba kabla au baada ya adhana, au awe na shaka juu ya hilo.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
Tafadhali ingiza thamani

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • Timsahın saxlanılması və digər ölkələrə satışına icazə varmı?
  3205 دیگر آبزیان 2014/05/22
  Təqlid olunan müctehidlərin cavabları bunlardır: Həzrət ayətullah Xamnei (Allah qorusun) Əti haram olan heyvanların saxlanılması və onun hətta, bu heyvanların ətlərinin yeyilməsini halal bilənlərə də satılması düzgün deyildir. Amma, aqillər nəzərində halal mənfəətə görə olsa məsələn, ətinin başqa ət yeyən heyvanlar üçün istifadəsi yaxud, dərisinin dəri sənətində ...
 • Batasan pakaian bagi perempuan untuk mengerjakan salat
  2399 پوشش 2015/04/18
  Batasan wajib menutup aurat bagi perempuan adalah menutup seluruh badan termasuk rambut kecuali wajah (seukuran dengan basuhan ketika berwudhu), kedua telapak tangan dan kedua kaki sampai pergelangannya. Dari sisi ukuran kainnya, maka kain itu harus bisa menutupi badan artinya seukuran dengan badan dan rambutnya tidak kelihatan. ...
 • iwapo amri za baba zitapingana na za mama, mwana atakuwa na anawajibu gani katika hali kama hiyo?
  7070 نیکی به پدر و مادر 2012/05/23
  Miongoni mwa amri kuu alizoamriswha mja na Mola wake baada ya ile amri ya kumpwekesha Mola wake, ni kwatii wazazi wawili. Kuhusiana na swali lililoulizwa hapo juu, pamoja na hali halisi iliyotajwa ndani ya swali hilo, mtu anapokuwa amekabiliwa na hali kama ...
 • jee mwanaadamu ni mwenye uhuru katika matendo yake? Na kama yeye ni mwenye uhuru, basi mipaka ya uhuru wake ikoje?
  4270 Elimu ya zamani ya Akida 2012/05/23
  Mara nyingi mwanaadamu akiwemo katika msafara wa maisha yake binafsi, hujikuta akiwa ni mpweke na mgeni ndani ya msafara huo. Lakini hakuna budi kila mmoja wetu kuwemo ndani ya msafara huo. Ukiizingatia vizuri njia ya msafara wako, utaikutia kuwa: ndani yake huwa mna mambo yaliyokuwa tayari yameshathibitika ...
 • nini siri hasa ya Uslamu kuwa ni dini ya mwisho, na nini pingamizi hasa ya bwana Surush juu ya hilo?
  6579 اسلام و ایمان 2014/02/12
  Kuzingatia nukta zifuatazo kutaweza kumsaidia msomaji kulitambua vyema suala hili: 1- Hitimisho la utume lina maana ya hitimisho la dini; na hii inamaanisha kuwa hakutokuja mtume mwengine baada Yake (s.a.w.w). Hayo pia utayakuta kwenye Aya ya 40 ya Suratul-Ahzab. 2- Dini ya Kiislamu imeitwa dini ya mwisho ...
 • nini maana ya ucha Mungu?
  10153 تقوی 2012/05/23
  Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
 • je kuutangaza mwezi ni jukumu la wanazuoni wote kwa ujumla, au ni jukumu tu la kiongozi (mwanafiqhi / kadhi) mkuu wa dini nchini?
  5381 رؤیت هلال و یوم الشک 2012/05/23
  Fani ya Fiqhi iliyo katika nyanja za juu (iliyobobea), huwa inampa mtu uwezo maalumu wa kuzivua na kuziopoa hukumu kuu za kisheria kutoka katika machimbuko yake, ambayo miongoni mwayo ni zile ibara za Qur-ani na Hadithi takatifu, na jambo hilo (kuwa na uwezo wa kuziopoa hukumu) ni ...
 • Nini maana ya Feminism?
  8192 Sheria na hukumu 2012/05/23
  Neno (Feminism) linatokana na lugha ya Kifaransa ambalo asili yake ya Kilatini ni (Femind), neno hili hutumika katika lugha mbali mbali huku likiwa na maana moja inayomaanisha uke au jinsia ya kike, ijapokuwa neno hili linapotumika kutoka lugha moja kwenda nyengine huonekana kuwa na mabadiliko kidogo ya ...
 • nini hukumu ya kufuga njiwa ndani ya sheria za Kiislamu? Na nini msingi hasa wa hukumu hiyo?
  14925 نگهداری و شکار حیوانات 2012/06/17
  Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
 • je ni kweli kuwa Malaika wameumbwa kupitia nuru ya Maimamu (a.s)? Na je ni kweli kuwa wadhifa wao ni kumlilia na kuomboleza mauwaji ya Imamu Husein (a.s)?
  8299 عزاداری و زیارت 2012/05/23
  1- Suala la Malaika kuumbwa kutokana na nuru ya watu fulani, ni suala maarufu lilinukuliwa kutoka kwenye Riwaya za pande zote mbili, za Masunni na Mashia. Ndani ya vitabu vya Kishia, kuna Riwaya zinazoelezea kuwa: Malaika wameumba kutokana na nuru za watu maalumu, kama vile: Mtume na ...

YALIYOSOMWA ZAIDI

MAFUNGAMANO