advanced Search

Kwa mara ya kwanza kabisa tovuti ya Islamquest ilianza kazi yake mnamo tarehe 2/4/2006, ambapo tovuti hii ilianza kutoa huduma zake kupitia lugha ya KIpashia, Kiarabu na Kiingereza.
   Lengo hasa la kuanzishwa kwa tovuti hii, ni kubeba jukumu la kujibu maswali mbali mbali yanayohusiana na dini ya Kiislamu kupitia njia ya mtandao wa internet.
Toleo la kwanza la tovuti hii liliweza kukamilika chini ya juhudi kubwa zilizofanywa na kikundi cha vijana mahodari wenye misingi madhubuti ya dini waliojitolea kuitekeleza kazi ya uundaji wa tovuti hii.
 

    Leo tovuti ya Islamquest imeweza kutoa huduma zake kupitia lugha kumi na nne tofauti za kimataifa, utowaji wa huduma hizi umetimia kupitia kundi kubwa la wahakiki na wafasiri mahodari walioweza  kutayarisha jawabu za zaidi ya maswali ishirini elfu kwa ajili ya maelfu ya wale wenye utashi wa kutaka kuufahamu Uislamu vilivyo. Toleo jipya la tovuti hii limetayarishwa na kikundi maalumu cha waumini hodari waliofanya juhudi za usiku na mchana zilizozaa tovuti hii yenye sura mpya iliyokuwa na uwezo wa hali ya juu katika kukidhi haja za watumiaji wa tovuti hii wakiwemo wale wenye kujibu mswali mbali mbali yanayoulizwa na wale wenye utashi wa kutaka kuelewa uhakika kamili wa Uislamu ulivyo.
   Taasisi yetu ijulikanayo kwa jina la Ukumbi wa Hekima, iko tayari kutoa bure kabisa program (software) ya tovuti hii iliyogharamia kiwango kikubwa cha fedha, na kukipa kitengo chechote kile chenye nia ya kutaka kutoa msaada wa kujibu maswali mbali mbali kupitia mtandao wa internet.
    Twataraji Mola atatuwafikisha tuwe ni mawakala wenye sifa kamili katika uwanja wa mtandao wa internet kwa ajili ya kusambaza na kuyatambulisha madhehebu bora ya Ahlul-Bait (a.s), pamoja na kuyatafutia jawabu tosha na za haraka yale maswali mengi yanayoulizwa katika ulimwengu wetu huu wa leo.
Mkuu wa taasisi ya Ukumbi wa Hekima


         MAHDI HADAWIY TEHRANIY
 

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI