advanced Search
KAGUA
5042
Tarehe ya kuingizwa: 2012/05/21
Summary Maswali
kwa nini tuwe wakalidi (wafuasi)?
SWALI
kwa nini tuwe wakalidi (wafuasi)?
MUKHTASARI WA JAWABU

Ruhusa ya kumfuata ulamaa maalumu katika matendo ya ibada za kila siku, inatakiwa kutolewa na akili ya mtu mwenyewe. Na wala ruhusa hiyo haingojewi kutoka kwa Maulamaa, huku kila mmoja akielewa umuhimu wa suala hili ndani ya maisha yake ya kila siku.

Katika hali yakawaida, mtu huwa ana sababu mbili zinanomfanya yeye kuwa ni mfuasi wa mtu maalumu:

1: Mwenendo wa kila mwenye akili huwa ni kuyatenda matendo yake kwa kupitia uoni wa kielimu aliokuwa nao, na pale anapohisi kuwa elimu yake ni changa kuhusiana na tendo analolitaka kulitenda, huwa anamuelekea mwerevu anayeutambua uhakika wa tendo hilo. Na mfano hilo ni kama vile mgonja kuenda kwa mtibabu ili amfafanulie ukweli wa magonjwa yake pamoja na kumpatia tiba ya magonjwa alionayo. Na hilo ndilo linalomfanya kila mwenye akili kumfuata ulamaa maalumu ili kupata ufafanuzi wa matendo na wadhifa wa kidini unaomuwajibikia yeye kisheria.

 

2: Kila muislamu anafahamu tosha kuwa dini yake ina maamrisho na makatazo maalmu yanayotakiwa kuzingatiwa na kila mfuasi wa dini hiyo, na ufahamu huu huwa ni dalili tosha itakayomfanya yeye kujihisi kuwa anawajibika kuyenda matendo yake kwa mujibu wa makatazo na maamrisho hayo yalivyo. Hapo ndipo anapojikuta kuwa; hana budi kufuata moja kati ya njia zifuatazo:

A: Awe na elimu ya kutosha itakayomuezesha kuyatambua maamrisho na makatazo hayo.

B: Awe na tahadhari katika matendo yake yote bila ya kufanya kosa katika uchaguzi wa matendo yake, yaani aliache kila lenye shaka na alishike kila lenye uhakika au kudhaniwa kuwa ni la sawa.

C: Awe ni mfuasi wa mwanachuoni maalumu, na matendo yake yawe yanaiegemea elimu  na mitazamo ya mwanachuoni huyo katika matendo yake yote ndani ya maisha yake ya kila siku.

 

Mtu ataposhikamana na moja kati ya njia hizi tulizozitaja, atajihisi kuwa ameyatekeleza matakwa ya dini  pamoja na wajibu wake ipaswavyo. Lakini njia ya mwazo huwa inahitajia muda mrefu ili yeye abobee kielimu, na kabla ya kuifikia daraja hiyo bila shaka atakuwa ni muhitaji wa moja kati ya njia mbili zilizobakia. Na njia ya pili nayo inahitajia mtu kuzielewa aina za haramu na halali pamoja na kuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na hoja tofauti za wanazuoni mbali mbali kutokana na nyadhifa zinazomkabili, na hilo si jambo jepesi liwezalo kupatikana kirahisi au kufikiwa na kila mmoja. Njia pekee iliobakia ni njia ya tatu. Kwa ufafanuzi zaidi tunatakiwa kuelewa kwamba; dalili namba mbili iliopita hapo juu, inaonesha ulazima wa kumfuata mwanachoni katika masuala yote yanayodhaniwa kuwa ni wajibu au haramu pamoja na yale yanayodhaniwa kuwa ni sunna iwapo mtu atapendelea kuzitenda sunna hizo, lakini dalili namba moja inalithibitisha na kulizingatia suala la ufuasi katika aina zote za matendo. La muhimu kufahamu hapa ni kwamba suala la mtu kuweza kubakia kuwa ni mfuasi wa ulamaa wake baada ya kufa kwa mwanachuoni huyo, huwa linahitajia fatwa ya ulamaa huyo kuhusiana na suala hilo ndani ya uhai wake, iwapo yeye atakuwa hakutoa fatwa au haruhusu mtu kumfuata ulamaa wake baada ya kufariki kwake, hapo basi itambidi mtu mwenyewe ambaye ni mfuasi, kuwa na uangalifu juu ya suala hilo katika kuepukana nalo au kubakia kuwa ni mfuasi wa ulamaa wake.

Bado kuna dalili nyengine zinazohisiana na masuala ya ufuasi, lakini jukumu la kuzisimamisha dalili hizo litabakia mikononi mwa maulamaa, kwani wao ndio wajuzi zaidi wanaoutambua vyema uwanja huu.

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • Shakhsiya yake ilikuwa vipi ?mtazamo wa Ahlul bait kuhusiana na yeye.Riwaya zilizonukuluwa kwake zina hukumu gani?
  2118 تاريخ بزرگان
  Umayri bni Maliki ni katika wajukuu wa khazraji aliyejulikana sana kwa vinyongo,ni katika sahaba wa mtume,[saww]yeye nikatika kabila la watu wa khazraj na aliishi Madina, alisilimu baada ya kupita miezi kadhaa ya mtume kufika Madinah Abu dardaii aliitikadi ubora wa imamAli[as] dhidi ya Muawiyah.Alifatana na Abu Huraira ...
 • Nini maana ya Feminism?
  10996 Sheria na hukumu
  Neno (Feminism) linatokana na lugha ya Kifaransa ambalo asili yake ya Kilatini ni (Femind), neno hili hutumika katika lugha mbali mbali huku likiwa na maana moja inayomaanisha uke au jinsia ya kike, ijapokuwa neno hili linapotumika kutoka lugha moja kwenda nyengine huonekana kuwa na mabadiliko kidogo ya ...
 • nini ilikuwa hatima ya farasi wa Imamu Husein (a.s) huko Karbala?
  5437 حوادث روز عاشورا
  Waandishi mbali mbali wa walioandika na kulizungumzia tokeo la Karbala, hawakutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na farasi wa Imamu Husein (a.s), bali walichokielezea ni kuwa, farasi huyu alijipakaa damu ya Imamu Husein (a.s), kisha akaelekea kwenye mahema huku akitoa sauti kali yenye kuashiria huzuni na hasira. Watu ...
 • nini maana ya neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر) lililonasibishwa na Mungu ndani ya Qur-ani?
  14579 مکر
  Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...
 • nini maana ya neno (dini)? Au dini hasa ni kitu gani?
  37760 Falsafa ya Dini
  Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
 • ni zipi funga zilizo zisizofaa kwa mtazamo wa imam Shafi, Hanafi na Maalik?
  11387 روزه های مستحب، مکروه و حرام
  Masiku yasiyofaa kufunga saumu mbele ya imam Abu Hanifa ni: siku ya idi ndogo na idi kubwa, pia kufunga siku ya mwezi 11, 12 na 13 ya mwezi wa Dhil-hijja, pia kufunga ndani ya idi pili hadi nne za idi ya mfunguo tatu. Funga zisizofaa ...
 • nini hukumu ya kupiga sindano ya nguvu au kutia maji ya nguvu (Intravenous injection) mwilini ndani ya Ramadhani?
  7265 گوناگون
  Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo: Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: ...
 • Shin aure yana da wasu sharaDai na musamman?.
  2804 Sheria na hukumu
  A mahangar musulunci auren da’imi da na mutu’a suna da sharaDai waDanda sune kamar haka:- 1. Karanto siga (Yarjewa juna tsakanin miji da mata shi kaDai bai wadatar ba lalle ne a hada shi da furta “farar da” lafazi na musamman). 2. Bisa ihtiyaDi na wajibi ya ...
 • Qur-ani ni muujiza wa mtume wa mwisho (s.a.w.w), muujiza wake basi uko katika hali gani?
  8310 Elimu za Qur-ani
  Kuna hali tatu za kimiujiza zilizotajwa kuhusiana na muujiza wa Qur-ani: muujiza unaohusiana na maneno ya Qur-ani, muujiza wa yale yalioomo ndani yake na muujiza wa Yule aliyekuja na Qur-ani (s.a.w.w) Muujiza unaohusiana na maneno ya Qur-ani umegawika katika sehemu mbili:
 • Timsahın saxlanılması və digər ölkələrə satışına icazə varmı?
  4717 دیگر آبزیان
  Təqlid olunan müctehidlərin cavabları bunlardır: Həzrət ayətullah Xamnei (Allah qorusun) Əti haram olan heyvanların saxlanılması və onun hətta, bu heyvanların ətlərinin yeyilməsini halal bilənlərə də satılması düzgün deyildir. Amma, aqillər nəzərində halal mənfəətə görə olsa məsələn, ətinin başqa ət yeyən heyvanlar üçün istifadəsi yaxud, dərisinin dəri sənətində ...

YALIYOSOMWA ZAIDI