advanced Search
KAGUA
9252
Tarehe ya kuingizwa: 2012/04/10
Summary Maswali
iwapo kwenye ngozi ya mwanamke kutakuwa na alama au athari fulani, je inajuzu mke huyo kuifanyia upresheni ngozi ya mwili wake baada ya mumewe kuliridhia jambo hilo? Kwani katika zama zetu hizi ni rahisi kuziondoa alama hizo kupitia kifaa maalumu chenye mwanga, mwanga ambao huwa unafanya kazi ya kuzifuta alama hizo kupitia wataalamu maalumu hospitalini.
SWALI
kwa kweli mimi nina ngozi yenye kuchukiza mno. Juu ya ngozi yangu kuna vidoto vya rangi ya kahawia, nami nimefanya juhudi kupitia madawa mbali mbali ili kuviondoa vidoto hivyo bila ya kufanikiwa, ama hivi sasa nimepata fursa maalumu ya kuvitokomeza vitodo hivyo kupitia njia ya upresheni wa mwanga, ingawaje njia hii itanigharamikia pesa nyingi, lakini mimi niko tayari kutoa gharama hizo. Ila tu mimi nataka kujua, je jambo hili linafaa? Huku tukizingatia kuwa tayari mimi nimeshashauriana na mume wangu, naye ameshanikubalia kufanya hivyo.
MUKHTASARI WA JAWABU

Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Khamenei (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu hii:

Iwapo wewe utakuwa katika mashaka makubwa kwa kutokana na kuwa na aina hiyo ya ngozi, basi unaruhusiwa kufanya upresheni kwa ajili ya kuitibu ngozi yako.

Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Makaarim Shirazi (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu ifuatayo:

Iwapo jambo hilo halitapelekea kutendeka jambo la haramu ndani yake, au kusababisha madhara mengine makubwa zaidi kulikoa haya aliokuwa nayo, hapo hapakutakuwa na tatizo, lakini iwapo kufanya hivyo kutapelekea kupatikana jambo fulani la haramu, kama vile kuguswa mwili wake au kukashifiwa na madokta, basi katika hali kama hii yeye hatoruhusiwa kufanya hivyo mpaka pale ambapo yeye atakuwa amelazimika kufanya hivyo kwa njia moja au nyengine, hapo tena yeye atakuwa hana budi kufanya hivyo.

JAWABU KWA UFAFANUZI

Namba maalumu ya kuelekea kwenye uwanja wa masali na majibu ya kifiqhi, ni 1994.

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI