A mahangar musulunci auren da’imi da na mutu’a suna da sharaDai waDanda sune kamar haka:- 1. Karanto siga (Yarjewa juna tsakanin miji da mata shi kaDai bai wadatar ba lalle ne a hada shi da furta “farar da” lafazi na musamman). 2. Bisa ihtiyaDi na wajibi ya ...
Fani ya Fiqhi iliyo katika nyanja za juu (iliyobobea), huwa inampa mtu uwezo maalumu wa kuzivua na kuziopoa hukumu kuu za kisheria kutoka katika machimbuko yake, ambayo miongoni mwayo ni zile ibara za Qur-ani na Hadithi takatifu, na jambo hilo (kuwa na uwezo wa kuziopoa hukumu) ni ...
Tokeo hilo linaweza kutokea katika sura tatu, nasi tutazifafanua sura hizo na kuzijibu kwa mujibu mitazamo ya maulamaa isemavyo. Na jawabu zetu ni kama ifuatavyo: 1- iwapo mtu ataacha kufunga kwa kutokana na maradhi, kisha maradhi hayo yakaendelea hadi akafikiwa na Ramadhani ya mwaka wa ...
Wanazuoni wote wa Kifiqhi wanasema kuwa: ni wajibu wa kila mwenye funga kuchukuwa tahadhari, na kutofikisha kitu chochote kile kama vile tumbaku au moshi wa sigara ndani ya koo yake.[1] Na hakuna hata mmoja miongoni mwa wanazuoni aliyetoa ruhusa ya kuvuta sigara ...
Mitazamo ya maulamaa ni yenye kutofautiana kuhusiana na suala hili. Moja kati ya mitazamo hiyo, ni ule mtazamo unaowafikiana na baadhi ya Riwaya pamoja na vitabu vya Tarehe, mtazamo huu ni kama ifuatavyo: mwili wa Imamu Husein (a.s), umezikwa na mwanawe mpenzi na muaminifu, naye ni Imamu ...
Kwa mujibu wa nukuu za baadhi ya Hadithi ni kwamba, majina ya matano ya Aali Abaa (a.s), yaani Aali wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambao ni: Ali, Fatima,Hasan na Husein, yametajwa ndani ya Taurati na Injili. Pia suala hilo linaonekana kuashiriwa ndani ya ile Hadithi yenye kunukuu majadilianao ...
Kila mwaka wa Hijiria kwa kawaida huwa una miezi kumi na mbili, na masiku ya miezi huwa yanahesabiwa kwa kuonekana kwa mwezi, hii ni kanuni ya mwaka wa Hijiria, ama mwaka Shamsia kwa kawaida masiku yake huwa tayari yameshatambulikana, na suala la kuonekana kwa mwezi si suala ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Kuzingatia nukta zifuatazo kutaweza kumsaidia msomaji kulitambua vyema suala hili: 1- Hitimisho la utume lina maana ya hitimisho la dini; na hii inamaanisha kuwa hakutokuja mtume mwengine baada Yake (s.a.w.w). Hayo pia utayakuta kwenye Aya ya 40 ya Suratul-Ahzab. 2- Dini ya Kiislamu imeitwa dini ya mwisho ...
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...