Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale yote yanayo dhaniwa kuwa ni maasi. Taqwa ni yenye daraja na vigao mbali mbali, pia natija na matunda ya taqwa ni yenye kutafautia. Ili kuutambua ufafanuzi kamili wa swali lako, basi tunakusihi usome jawabu kamili ya swali hili inayo fuata hapa chini.
Neno “taqwa” ni neno la Kiarabu linalo tokana na mzizi wa neno “Wiqaayatun” na serufi ya neno hilo ni "وقی یقی وقايه", neno hili lina maana ya kule mtu kujilinda kupitia kitu au ngao fulani.[1] Na katika fani ya dini, neno hili kitaalamu, lina maana ya kule mtu kujiweza au kuimiliki nafsi yake, kunakomfanya yeye awe nje ya maasi au ajitenge na maasi.
Kwa ibara nyengine ni kwamba: taqwa ni zile nguvu maalumu ambazo hugeuka kuwa ni kipaji kilichomo ndani ya nafsi ya mwanaadamu alichojichumia mja kupitia fikra na matendo maalumu, nguvu ambazo humuezesha yeye kuimiliki nafsi yake pale anapo kutana na vishawishi au pale nafsi yake inapotaka kumuelekeza katika maasi kwa namna moja au nyengine. Taqwa iliyo kamilika, haimuezeshi tu mja kujiepusha na madhambi pamoja na yale yaliyo haramishwa, bali pia inamfanya yeye kujitenga na yale mambo yenye mashaka, ambayo ndani ya uwanja wa akili madhubuti, hudhaniwa kuwa ni mambo yasiyo takikana kutendwa.
Katika Aya na Hadithi mbali mbali, imetolewa mifano mbali mbali kuhusiana na taqwa, na miongoni mwayo ni kama ifuatavyo:
(Enyi waja wa Mungu, taqwa ni ngome madhubuti isiyo penyeka).[4]
Taqwa ni kimurimuri chenye kuashiria kuwepo kwa imani juu ya Muumba na siku ya malipo.[8]
Kwa mtazamo wa Qur-ani, taqwa ni nuru itokayo kwa Mola Mtukufu, na popote pale iangazapo nuru hiyo, basi hupatikana ongezeko la elimu na maarifa.[9]
Daraja mbali mbali za taqwa
Taqwa ni yenye daraja mbali mbali. Baadhi wacha Mungu wameigawa taqwa katika daraja tatu zifuatazo:
Vitawi vya taqwa
Taqwa ina aina mbali mbali za vitawi, na miongoni mwa vitawi ambavyo vinaweza kuashiriwa kirahisi kabisa, ni kama ifuatavyo: taqwa kwenye mali na uchumi, taqwa katika masuala ya kijinsia, taqwa ndani ya kijamii, taqwa ya kisiasa na taqwa katika maadili binafsi. Mwenye taqwa anatakiwa kuitumia taqwa yake binafsi katika kuyachunga mambo yote tuliyoyataja hapa.
Matunda ya taqwa
Taqwa ni yenye matunda mbali mbali adimu katika maisha ya binaadamu, na miongoni mwayo ni kama ifuatavyo:
Hayo yote tuliyo yazungumza na kuyafafanua kwa namna mbali mbali ni mambo msingi katika mtu kupata muelekeo sahihi. Huu basi ni mlolongo wa ibara zenye maelekezo kamili kuhusiana na swali lililo ulizwa hapo juu, yaani swali juu ya maana halisi ya neno “taqwa”.
[1] Angalia neno "وقی" katika kitabu Mufradaatu-fi-Ghariibil-Qur-ani, cha Husein bin Muhammad Isfahaniy, juz/1, uk/881, chapa ya Daarul-Ilmi Damascus na Al-Daarush-Shaamiya, Beirut Lebanon.
[2] Suratul-baqara, Aya ya 197.
[3] Suratul-Aa’raaf, Aya ya 26.
[4] Nahjul-Balagha, hutuba ya 157.
[5] Nahjul-Balagha, hutuba ya 16.
[6] Raudhatul-Jinaan-wa-Ruhul-Jinaan-fi-Tafsiril-Qur-ani, cha Husein bin Ali, juz/1, uk/102, chapa ya Buniaad Pazjuuheshhaye Islaaamiy Astaane Qudsi Radhawiy, Mash-had, Iran, mwaka 1408. Tafsiri Nemune ya Nasir Makaarim Shiraziy, juz/1, uk/80, chapa ya kwanza ya Darul-Kutubil-Islaamiyya, Tehran, mwaka 1374 Shamsia.
[7] Tafsiri Nemune ya Nasir Makaarim Shiraziy, juz/22, uk/204.
[8] Suratul-Hujurati Aya ya 14.
[9] Suratul-Baqara, Aya ya 282.
[10] Tafsiri Nemune ya Nasir Makaarim Shiraziy, juz/22, uk/205. Biharul-Anwaar, cha Allaama Majlisy, juz/70, uk/136, chapa ya Alwafaa, Beirut Lebanon, mwaka 1404 Hijiria.
[11] Khutbatul-Muttaqiin, ilioko ndani ya kitabu Nahjul-Balagha.