Tukitoa jawabu ya kiujumla jamala kuhusiana na swali hilo lililoulizwa hapo juu, tunasema kuwa: si katika zama za zamani au za hivi sasa tu, bali katika zama zote hakujawahi kutokea mtu aliyeweza kuja na maneno yenye kufanana na Qur-ani kiufasaha na kibalagha, bali ufasaha unao onekana ndani ...
Suala la kuonekana kwa mwezi ni lenye umuhimu ndani ya miezi yote, lakini suala hilo huwa ni lenye kupewa kipau mbele zaidi ndani ya mwezi wa Ramadhani, kwa kutokana na ulazima wa ibada ya funga iliyomo ndani yake, ambayo ni ya wajibu kwa Waislamu wote, pia suala ...
Imamu Husein (a.s) pamoja na wafuasi wake pale walipokuwa Karbala, walikuwa wakisoma mashairi maalumu yenye ibara za kivita, kwa ajili ya kuwahamasisha wanavita, pia Abul-Fadhlil-Abbaas alionekana mara zote katika siku ya Ashura kusoma aina mbali mbali za ibara na mashairi ya kuvutia kwa ajili ya uhamasishaji, mashairi ...
Kwa kweli kisheria hakuna matatizo yoyote yale kuhusiana na suala hilo la mtu kuwa na aina mbili za kazi au madaraka. Ndio Uislamu umewatahadharisha watu kuhusiana na kuwa na mapenzi makubwa ya kuipenda dunia na kuyasahau maisha ya Akhera, dlakini mtu anaweza akawa na aina mbili za ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Wakristo walipokuwa wakiishi katika zama ambazo Isa (a.s) alikuwa tayari ameshapaishwa mbinguni na Mola wake, jukumu la kulingania dini lilishikwa na mitume pamoja na wafuasi wake (Hawariyyuun), waliokuwepo kwa ajili yake ndani ya zama hizo, na licha ya mitume na wafuasi hao kupata adhabu mbali mbali pale ...
Wajukuu hawa wawili wa Mtume (s.a.w.w) ni mabwana wenye utukufu juu ya vijana wote Peponi, haidhuru kuwa ndani ya Pepo watu wote watakuwa katika hali moja ya ujana, ama wao (Imamu Hasan na Husein (a.s)) ndio watakaong’ara zaidi katika wale vijana waliouwawa katika njia ya Mola, au ...
Təqlid olunan müctehidlərin cavabları bunlardır: Həzrət ayətullah Xamnei (Allah qorusun) Əti haram olan heyvanların saxlanılması və onun hətta, bu heyvanların ətlərinin yeyilməsini halal bilənlərə də satılması düzgün deyildir. Amma, aqillər nəzərində halal mənfəətə görə olsa məsələn, ətinin başqa ət yeyən heyvanlar üçün istifadəsi yaxud, dərisinin dəri sənətində ...
Ruhusa ya kumfuata ulamaa maalumu katika matendo ya ibada za kila siku, inatakiwa kutolewa na akili ya mtu mwenyewe. Na wala ruhusa hiyo haingojewi kutoka kwa Maulamaa, huku kila mmoja akielewa umuhimu wa suala hili ndani ya maisha yake ya kila siku. Katika hali yakawaida, ...
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...