Miongoni mwa amri kuu alizoamriswha mja na Mola wake baada ya ile amri ya kumpwekesha Mola wake, ni kwatii wazazi wawili. Kuhusiana na swali lililoulizwa hapo juu, pamoja na hali halisi iliyotajwa ndani ya swali hilo, mtu anapokuwa amekabiliwa na hali kama ...
Kwanza tuwie radhi kawa kuchelewa kukujibu swali lako. Tuna tazizo wakati mwengine la kuchelewa kujibu maswali kwa haraka, hii ni kwa kutokana na kuzidiwa na maswali, au wafanya kazi wetu kuto kuwa na muda wa kutosha katika kujibu maswali mbali mbali. ...
Hadhithi Kisaa (Hadithi ya joho) ambayo imenukuliwa ndani ya kitabu cha Sheikh Abbas Qummiy kijulikanacho kwa jina la Mafaatiihul-jinaan, ni Hadithi iliyobeba ndani yake ujumbe mzito wenye umuhimu wa aina mbili. Umuhimu wa kwanza ni kule Hadithi kuwa na fungamano la moja kwa moja na suala la ...
Jawabu kutoka ofisi ya elimu ya AyatuLlahi Khamenei (Mungu amhifadhi): Iwapo kumfunga huko mimba kutakuwa ni mateso kwa mnyama huyo, basi jambo hilo halitofaa kutendwa. Jawabu kutoka ofisi ya elimu ya AyatuLlahi Mahdi Hadawiy Tehraniy (Mungu amhifadhi), ni kama ifuatavyo: Iwapo ...
Wanazuoni wa Kifiqhi wanasema kuwa: mtu atakayeiharibu funga yake kwa makusudi, antakiwa ima amtowe huru mtumwa,[1] au afunge miezi miwili mfululizo, au awalishe mlo mmoja maskini sitini mpaka washibe, au ampe kila mmoja kati yao kiwango cha gramu 750 ya nafaka ambayo inatambulikana kuwa ...
Wanazuoni wote wa Kifiqhi wanasema kuwa: ni wajibu wa kila mwenye funga kuchukuwa tahadhari, na kutofikisha kitu chochote kile kama vile tumbaku au moshi wa sigara ndani ya koo yake.[1] Na hakuna hata mmoja miongoni mwa wanazuoni aliyetoa ruhusa ya kuvuta sigara ...
Ndani ya Qur-ani na Riwaya mbali mbali, kuna mafunzo mbali mbali yenye kuwafahamisha waja masharti ya mwanzo yanayosababisha kukubaliwa amali zao, na masharti msingi yaliyotajwa katika mafunzo hayo ni kumuamini Mola, kujiepusha na shirki pamoja kuto ritadi, na bila ya kuwepo misingi hiyo Mola hatozikubali aina zozote ...
Si tatizo mtu kumpa chakula wakati wa mchana muislamu asiyefunga ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hukumu hii na kwa yule muislamu amedharurika kufunga. Kama vile kumpa chakula wakati wa mchana muislamu aliye mgonjwa au msafiri. Kwa upande wa pili; ni vyema kutompa chakula muislamu asiyeruhusika kula (asiye ...
Imamu Khomeiniy (r.a), alitilia mkazo sana katika mazungumzo yake ya mara kwa mara ya kwamba: muhanga wa Imamu Husein (a.s), pamoja kuadhimisha siku ya muhanga huo kwa kuandaa vikao vya maombolezo kwa ajili ya kuikumbuka kwa ajili ya kupata somo juu ya tendo hilo la Imamu Husein ...
Ofisi ya kielimu ya Ayatu-Llahi Khamenei (Mungu amhifadhi) yenye kuhusika na kujibu maswali ya kifiqi, imetoa jawabu hii: Iwapo wewe utakuwa katika mashaka makubwa kwa kutokana na kuwa na aina hiyo ya ngozi, basi unaruhusiwa kufanya upresheni kwa ajili ya kuitibu ngozi yako.
Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
iwapo mtu atawajibikiwa kufunga mwezi wa Ramadhani, naye kwa makusudi akabakia na janaba hadi adhana ya asubuhi, anaweza yeye akatayamamu katika nyakati za mwisho kabisa kabla ya kuadhiniwa adhana hiyo badala ya kuoga, kwa kuwa wakati wa kuoga haupo tena, kisha aendelee na funga yake, na funga ...
Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...
Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...