KAGUA
11192
Tarehe ya kuingizwa: 2006/06/03
Summary Maswali
nini maana ya neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر) lililonasibishwa na Mungu ndani ya Qur-ani?
SWALI
nini maana ya neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر) lililonasibishwa na Mungu ndani ya Qur-ani?
MUKHTASARI WA JAWABU

Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia  za kuyafikia mazuri au mabaya.

Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) kwa Mola Mtakatifu, na maana halisi ya neno hili ndani ya Aya hizo huwa  inamaanisha maana ya upangaji wa mambo kiujumla jamala, kwani Yeye Ndiye Mmiliki wa njia zote za upangaji wa mambo, na wala hakuna njia yeyote ile ya upangaji wa mambo iliyoko nje ya uwezo na milki yake. Hivyo basi Mola ni mwenye daraja ya juu kabisa katika suala la upangaji kuliko aina zote zile za wapangaji wa mipango mbali mbali, na hilo limezungumzwa ndani ya Qur-ani pale Mola Aliposema: «اللَّه خير الماكرين», yaani Mola ni Mbora wa wapangaji, na katika Aya nyengine Mola Anasema: (Kabla yao vile vile kulikuwako wakorofi waliopanga mipango na njia mbali mbali (za uharibifu), lakini njia na mipango yote iko ndani ya uwezo wa Mola. Na Mola yanamuelea yote yale yatendayo na kila mja, na muda si mrefu makafiri watatambua kuwa hatima njema itamfikia nani!). Aya hii inatoa upeo wa wazi kabisa kuwa, mipango yote ipo kwenye uwezo Wake Mola, na mipango ya wapangaji wengine haiwezi kuwa na nafasi mbele Yake.

JAWABU KWA UFAFANUZI

Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia  za kuyafikia mazuri au mabaya.[1]

Lakini neno hilo kwa wakati mwengine humaanisha kufanya ujanja na udanganyifu, vile vile neno hilo limenasibishwa na Mola huku likiwa na maana ya ujana na kuadhibu.[2]

 

"مكر الا لهى au ujanja wa Mola": tukiliangalia neno (مكر) namna lilivyokuja katika Aya tofauti za Qur-ani,[3] tutakutia kuwa neno hili limetumika ndani ya Qur-ani likiwa na maana ya upangaji wa mipango na utafutaji wa budi, lakini mara nyengi upangaji huo huwa ni kwa ajili ya kuleta madhara na wakati mwengine ukawa ni kwa ajili ya kuleta manufaa, kwa mfano katika Aya isemayo: «وَ يمكرون و يكمر اللَّه واللَّه خَير الماكِرين» yaani “wao ni wenye kupanga mipango kwa nia ya madhara, lakini Mola ni Mbora zaidi wa wapangaji wa mipango (iwe ya madhara au ya kuleta faida)”.[4] Maana ya wao kufanya ujanja kunamaanisha kule kupanga kwao mipango maalumu kwa ajili ya kumua Mtume (s.a.w.w) au kumuekea kwa vikwazo mbali mbali, na maana ya neno "يَمكُرُ اللَّهُ" humaanisha kule Mola kuwa ni mwenye kupanga mipango maalumu ambayo ilimuamuru Mtume (s.a.w.w) kuhamia Madina. Na kama utaiangaza Qur-ani kwa makini, utalikutia neno مكر)) ndani yake likipewa sifa ya ubaya kwa kuitwa السَّيِئّى)  مکر) jambo ambalo litakufahamisha kuwa kuna aina mbili za upangaji wa mipango, nazo ni upangaji wa mipango kwa ajili ya wema au manufaa na upangaji wa mipango kwa ajili ya madhara fulani.[5] La kuzingatia hapa ni kwamba pale neno hili linapotumika ndani ya Qu-ani huku likinasibishwa na Mola, huwa lina maanisha kuwa Mola Ndiye Aliye Mmiliki wa aina zote zile za upangaji, na wala hakutatokea njia au mipango itakayoweza kukaa njie ya uwezo na milki Yake (s.w). Na hiyo ndiyo maana ya kuwa Yeye yuko juu zaidi kuliko wapangaji wote wengine waliopo au wanaokadiriwa kuwepo.[6] Aya ilioko katika Surat Raad[7] iko wazi kabisa katika kuufikisha ujumbe huo unao onyesha kuwa: Yeye ndiye aliye miliki aina zote zile za upangaji, na wapangaji wengine wote hawana uwezo wowote ule mbele ya upangaji Wake Yeye (s.w).[8]

 

 


[1] Qamusi ya Qur-ani ya Sayyid Ali Akbar Qurashiy/ juz: 6/ uk: 265.

[2] Almunjid kilichotarjumiwa na Muhamed Bandar Rikiy, juz: 2/ uk: 1820.

[3] Rejea Suratul  Aaraaf Aya ya  99 na 123, Faatir 10 na 43,  Raad 33 na 42, Sabaa 33, Yuunus 21, Aal-Imraan 54, Nahl 26 na 45, Naml 50 na 51, Nuuh 22, Ibrahim 46, Yusuf 13 na Ghafir 45.

[4] Anfaa,l 30.

[5] Faatir, 43.

[6] Aali-Imraan, 54.

[7] Raad, 42.

[8] Tafsiri Al-miizaan ya Sayyid Muhamed Husein iliyotarjumiwa na Musawiy Hamadani/ juz: 12/ uk: 355, chapa ya Intishaaraat Islami.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • kwa nini tuwe wakalidi (wafuasi)?
  3857 تقلیدچیست؟ 2012/05/23
  Ruhusa ya kumfuata ulamaa maalumu katika matendo ya ibada za kila siku, inatakiwa kutolewa na akili ya mtu mwenyewe. Na wala ruhusa hiyo haingojewi kutoka kwa Maulamaa, huku kila mmoja akielewa umuhimu wa suala hili ndani ya maisha yake ya kila siku. Katika hali yakawaida, ...
 • nini hukumu ya kupiga sindano ya nguvu au kutia maji ya nguvu (Intravenous injection) mwilini ndani ya Ramadhani?
  5388 گوناگون 2012/05/23
  Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo: Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: ...
 • Vacip olan kaza orucu bozmanın hükmü nedir? Eğer kaza orucu tutan birisi eşiyle birlikte olursa orucu bozulurmu? Lütfen yardımcı olun.
  367 Miscellaneous questions 2019/01/23
  Orucu boazan unsurlar hakkında orucu bozan şeyler, soru:6047 (site:6217) adresine müracaat ediniz. Orucu bozan unsurlardan birisi cinsel ilişki olduğu için ramazan orucu veya kaza orucu arasında hüküm farklılığı yoktur. Yani oruç batıl olur. Ancak ramazan orucunun kazasını yerine getiren şahsın kazayı yerine getirmek için fırsatı varsa öğle ...
 • vipi madhehebu manne ya Ahlu-Sunna yalipatikana, na ilikuwaje mlango wa ijitihadi wa madhehebu hayo ukafungwa?
  15636 Sheria na hukumu 2012/06/17
  Mafunzo na fiqhi ya Kiislamu yaligawika sehemu mbili tokea ndani ya kipindi cha mwanzo cha tarehe ya Kiislamu baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w), kipindi ambacho kilikuwa ni kipindi cha mzozo katika suala la nani ashike ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w), hapo kukazaliwa aina mbili za fiqhi: ...
 • Vipi talaka hutimia, maneno gani hutumika kwa ajili ya talaka, na ni mara ngapi?
  469 طلاق 2018/11/10
  Kulingana na madhehebu ya Shia, iwapo mtu atakasirika kupita budi, kiasi ya kwamba akawa ametoa talaka bila ya makusudia au bila ya hiari kwa kutokana na kutawaliwa na hasira kupita budi. Hapo talaka haitakutimia. Ila kama atakuwa amekasirika kupitia budi, ila bado yupo timamu na akawa ametoa ...
 • Nini maana ya Feminism?
  8633 Sheria na hukumu 2012/05/23
  Neno (Feminism) linatokana na lugha ya Kifaransa ambalo asili yake ya Kilatini ni (Femind), neno hili hutumika katika lugha mbali mbali huku likiwa na maana moja inayomaanisha uke au jinsia ya kike, ijapokuwa neno hili linapotumika kutoka lugha moja kwenda nyengine huonekana kuwa na mabadiliko kidogo ya ...
 • Nini hukumu ya mwenye kumpa chakula muislamu asiyefunga?
  491 گوناگون 2018/11/05
  Si tatizo mtu kumpa chakula wakati wa mchana muislamu asiyefunga ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hukumu hii na kwa yule muislamu amedharurika kufunga. Kama vile kumpa chakula wakati wa mchana muislamu aliye mgonjwa au msafiri. Kwa upande wa pili; ni vyema kutompa chakula muislamu asiyeruhusika kula (asiye ...
 • nini hukumu ya funga kwa mjumbe anaye safiri kwa ajili ya kuufikisha ujumbe wa Alla (S.W) au kwa ajili ya kufanya kazi fulani?
  5138 شغل مسافرتی 2012/05/23
  watu kama hawa wanatakiwa kusali safari, na pia hawaruhusiwi kufunga katika hali kama hiyo, na wala hawawezi kufunga funga zao za nadhiri huku wakiwemo ndani ya mwezi wa Ramadhani tena safarini. Lakini iwapo wao wataifikia sehemu walioikusudia kwenda kubaki hapo kabla ya kukengeuka kwa jua, ...
 • Kodi za yanayohusiana na maudhui
  458 اعتکاف 2018/11/10
  Kwanza tuwie radhi kawa kuchelewa kukujibu swali lako. Tuna tazizo wakati mwengine la kuchelewa kujibu maswali kwa haraka, hii ni kwa kutokana na kuzidiwa na maswali, au wafanya kazi wetu kuto kuwa na muda wa kutosha katika kujibu maswali mbali mbali. ...
 • je dini na siasa ni vyenye kuendana au vyapingana?
  7481 Elimu mpya ya Akida 2012/05/23
  Dini ni chombo maalumu kilichokuja kumkomboa mwanaadamu na kumuongoza katika njia ya mafanikio, hivyo basi ni jambo lisiloingia akilini kuwa chombo hichi kiwe ni chenye kulipa mgongo jambo muhimu linalohitajika ndani ya jamii mbali mbali, kama vile suala la usimamishaji wa serikali. Na kwa upande mwengine ni ...

YALIYOSOMWA ZAIDI