advanced Search
KAGUA
8996
Tarehe ya kuingizwa: 2010/11/13
Summary Maswali
je hili shairi lisemalo: “mfalme wa wote ametupwa chini, na medali ya pambo (kichwa cha Imamu Husein) ikachokwa juu ya mshale, kichwa kile hakikuwa ni cha kawaida, bali ni shina na kibla kinachoelekewa na nyoyo zenye kufuata taa ya upendo” ambalo linadaiwa kuwa ni la Allaama Shaa’araniy, je kweli shairi hili linatokana naye?
SWALI
ndani ya vikao mbali mbali vya taazia na maombolezo ya Imamu Husein (a.s), huonekana kusomwa shairi linalosadikiwa kuwa linatokana na Allaama Shaa’raniy, huku maneno ya shairi hilo yakiwa na maana ifuatayo: “Mfalme wa wote ametupwa chini, hadi taji lenye kupendeza (kichwa cha Mimamu Husein (a.s) likaonekana kung’aa juu ya kichwa cha mshale, mara nuru ya medali yenye thamani itokanayo na taji hilo ikaupamba mshale huo kwa nuru isio na kifani…, kichwa kile hakikuwa ni kichwa tu kwenye jicho la yakini, bali ni shina na kibla kinachoelekewa na nyoyo zenye kufuata taa ya upendo”. Inaonekana sahiri hili limenukuliwa kutoka katika kitabu (Dam-us-sajuum) kitabu ambacho ni tarjama ya kitabu kijulikanacho kwa jina la (Nafsul-humuum), swali letu kuhusiana na suala hili ni kuwa je hivi kuna dalili na ishara yoyote yenye kuonesha kuwa shairi hilo ni la Allama Shaa’raniy? Na kama kuna dalili kuhusiana na hilo, basi tunaomba mutupe rejeo au rejea ya shairi hilo.
MUKHTASARI WA JAWABU

Kitabu (Dam-us-sajuum) ni tarjama ya kitabu maarufu cha maombolezo kinachotokana na Haaj Sheikh Abbaas Qummiyi, ambaye ni muandishi wa kitabu Mafaatihul-jinaan. Kitabu (Dam-us-sajuum) kimepigwa chapa na kitengo cha uchapishaji cha Hijrat kilichoko Qum Iran mwaka 1386 Shamsia, chini ya jina la (Dam-us-sujuum-fii-maqtal-Sayyidunal-Husein Madhluum (a.s)). Kitabu (Nafsul-humuum) asili yake kimeandikwa kwa lugha ya Kiarabu, na Allaama Shaa’raniy (r.a), ndiye aliyefanya kazi ya kukitarjumu kitabu hicho kutoka kwenye lugha ya Kiarabu kwenda Kifarsi, huku yeye akionekana kutoa baadhi ya ufafanuzi kwenye baadhi ya vipengele na ibara alizozifasiri au kuzitarjumu kutoka katika lugha mama ya kitabu hicho, na miongoni mwa zile ibara zilitolewa ufafanuzi na mfasiri huyu, ni hili shairi ambalo muulizaji wetu amelielekea na kuuliulizia uhakika wake na wapi yeye anaweza kupata nukuu za shairi hilo, na baadhi ya maana ya shairi hilo ni kama ifuatavyo:

Mfalme wa wote ametupwa chini, hadi taji lenye kupendeza (kichwa cha Mimamu Husein (a.s) likaonekana kung’aa juu ya kichwa cha mshale, mara nuru ya medali yenye thamani itokanayo na taji hilo ikaupamba mshale huo kwa nuru isio na kifani…, kichwa kile hakikuwa ni kichwa tu kwenye jicho la yakini, bali ni shina na kibla kinachoelekewa na nyoyo zenye kufuata taa ya upendo.

   Huu basi ndiyo ufafanuzi juu ya swali lako, tunataraji jawabu yetu itakuwa ni yenye kuwatosheleza wasomaji wetu kuhusiana na swali lililoulizwa hapo juu.

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI