Please Wait
8152
Kwa kweli hakuna kitabu miongoni mwa vitabu maarufu vya Tarehe vyenye kutegemewa kilichozungumzia na kuthibitisha suala la hali halisi juu ya wazee wa Maalik Ashtar, bali tu kinachofahamika kuhusiana nao, ni kuwa wao ni watu wa makabila ya (Nukha’a) na (Mudh-haj) yalioko huko Yemen, lililothibitika ndani ya Tarehe ni kwamba, makabila haya yalikuwa ni miongoni mwa makabila ya mwanzo yaliyoukubali na kuuamini Uislamu.
Maalik Ashtar alikuwa na watoto wawili wa kiume, mmoja alijulikana kwa jina la Is-haaq na mwengine Ibrahim. Is-haaq alikuwa ni mfuasi wa Imam Husein (a.s) aliyemuunga mkono Imamu Husein (a.s) kwenye mapambano ya Karbala, na hatimae kuuwawa katika mapambano hayo, na Ibrahim naye alikuwa ni mfuasi wa Ahlul-Bait (a.s), naye alishiriki katika mapambano yaliyotekea katika vugu vugu la kutaka kulipiza kisasi cha mauaji ya Imam Husein (a.s), vugu vugu ambalo lilianzishwa na Mukhtari Thaqafiy, huku Ibrahim akiwa ni miongoni mwa makamanda wa kivita ndani ya tokeo hilo, yeye aliifanya kazi yake kwa vizuri pasi na woga, na wengi miongoni mwa majahili waliomdhulumu Husein (a.s) walipata jaza yao ya kifo kupitia mkononi mwa Ibrahim, na mmoja miongoni mwa majahili muhimu alioweza kuwateketeza, ni Ibnu Ziad, ambaye alikuwa ndiye shetani mkuu dhidi ya Imamu Husein (a.s). vitabu vya Tarehe vinaelezea kuwa, Ibrahim alikuwa na watoto watano, nao ni: Nuuman, Maalik, Muhammad, Qasim na Khuulaan. Na miongoni mwa watoto hao watano, wapo watoto wawili ambao walikuwa ni wapokezi wa Hadithi, mmoja wao akiwa ni Muhammad na wa pili akiwa ni Qaasim.
Maalik bin Harith bin Abdu-Yaghuth bin Salma bin Rabia bin Harith bin Khuzaima bin Sa’ad bin Maalik bin Nukha’a, anatokana na koo mbili asili zilizo shujaa nazo ni Nukha' na Mudh-haj.[1] Yeye alizaliwa katika zama za kijahili kabla ya kuja kwa Uislamu,[2] ama kuhusiana na namna ya kusilimu kwake yeye mwenyewe au ukoo wake, ni moja ya mambo ambayo hayakufafanuliwa na vitabu vya Tarehe, na wala hakuna Hadithi au mfano wa Hadhithi uliolizungumzia suala hilo.[3] Baadhi ya waandishi wanakadiria kuwa yeye alisilimu pale Imamu Ali (a.s) alipokwenda Yemen kuutangaza Uislamu.[4] Kwani makabila mengi yaliukubali Uislamu na kusilimu makundi kwa makundi, kama vile kabila la Hamdaan, Nukha’a na Mudh-haj.
Katika zama za ukhalifa wa Abu Bakar, ukoo huu asili wa Kiarabu ulishika njia ya Sham (Siria) kisha ukaelekea Iraq kwenye mji maarufu ujulikanao kwa jina la (Kuufa), na hapo ndipo yakawa makazi ya kabila hilo, wao walizaliana na kukusanyika siku baada ya siku, hadi ukoo wao ukakua na kuota mizizi ndani ya mji huo. Kizazi cha maalik kilikua siku baada ya siku, na hatimae kizazi hicho kikazaa koo kubwa zilizojulikana kwa jina la (Banu Maalik), (Banu Ibrahim) n.k. Pia hadi leo kuna koo mbali mbali ambazo nasabu zake zinatokana na Maalik Ashtar, na miongoni mwa koo hizo ni Aalu Kaashiful-Ghitaa na Aalu Radhiy.
Imenukuliwa kutoka kwenye vitabu vya Tarehe kuwa, Maalik alikuwa na watoto wawili waliojulikana kwa majina ya Ibrahim na Is-haaq. Is-haaq alikuwa ni mfuasi mkereketwa wa Imamu Husein (a.s) ambaye alishika upanga katika vita vya Karbala baada tu ya kuuwawa kwa Habib bin Madhahir, na hatimae akauwawa katika vita hivyo.[5] Ibrahim alikuwa ni mtoto shujaa wa Maalik Ashtar, ambaye ni mpenzi na mfuasi shupavu wa Ahlul-Bait (a.s). Yeye alikuwa ni Shia madhubuti aliye makini kiimani na kimatendo, na hakufanana tu na baba yake kiimani na kimatendo, bali pia alifanana naye kimwili pamoja na sura.[6] Muandishi maarufu wa Tarehe ajulikanaye kwa umaarufu wa Dhahabiy, amenukuu kutoka kwa waandishi wa Tarehe wa madhehebu ya Kisunni akisema: “Ibrahim alikuwa ni shujaa kama baba yake aliyebobea sifa njema na alikuwa ni miongoni mwa watu watukufu”.[7] Ibrahim alishiriki mapinduzi muhimu yaliosimamishwa na Mukhtari Thaqafiy kwa nia ya kutaka kulipiza kisasi na kuwapandisha katika kiriri cha sheria wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyengine katika mauwaji ya Imamu Husein (a.s). Ibrahim waliweza kuwatokomeza maadui wengi wa Ahlul-Bait (a.s) ambao walishiriki katika mauaji ya Karbala, na miongoni mwa wale walioteketea kupitia mkononi mwake, ni Ibnu Zaid ambaye alimteketeza ndani ya siku ya kumi ya mwezi wa Muharram ya mwaka 67 Qamaria.[8] Vitabu vya Tarehe vimenukuu kuwa Ibrahim alikuwa na watoto watano waliojulikana kwa majina yafuatayo: Nuumani, Maalik, Muhammad, Qaasim na Khuulaan. Miongoni mwa watoto hawa, mna wale watoto wawili ambao walikuwa ni wapokezi wa Hadithi, nao ni Muhammd na Qaasim.[9]
Kwa ajili ya utafiti zaidi rejea: kitabu (A’ayani Shia) cha Sayyid Muhsin Amin, juz/2, uk/200, Daarut-Ta’ariif lilmatbuua’at, Beirut Lebanon, mwaka 1406 Qamaria.
[1] Dairatul-Maarif Shial- A’amma cha Muhammad Husein A’alamiyul-Haairiy, juz/16, uk/40, chapa ya pili ya Muasastul-A’alamiy lilmatbuua’at, Beirut, chapa ya mwaka 1413. Pia kitabu A’ayanush-Shia cha Sayyid Muhsin Al-Amin, juz/9, uk/38, chapa ya Dairatul-Ma’arif lilimatbuua’at, Beirut , chapa ya mwaka 1403. Pia kitabu Maalik Ashtar Khutabihi wa Aaraihi, cha Qeisul-Attaar, uk/13, chapa ya kwanza ya Muasasatul-Fikril-Islamiy Iran ya mwaka 1412.
[2] Rejea kitabu Al-A’alaam cha Khairud-Diin Al-Rarkaliy, juz/5, uk/259, chapa ya kwanza ya Daarul-Ilm, Beirut.
[3] Rejea kitabu Maalik Ashtar cha Sayyid Muhammad Ridha Al-Hakim, uk/33, chapa ya kwanza ya Maktabatul-Haidariyya Qum Iran, ya mwaka 1427.
[4] Rejea kitabu Maalik Ashtar cha Muhammad Muhammadiy Ishtihardiy, uk/19, chapa ya pili ya Intishaaraat Peyam Aazaadiy Tehran, mwaka 1372.
[5] Rejea kitabu Maalik Ashtar cha Muhammad Muhammadiy Ishtihardiy, uk/188.
[6] Dairatul-Maarif Shial- A’amma cha Muhammad Husein A’alamiyul-Haairiy, juz/2, uk/131.
[7] Seiru A’alaamin-Nubalaa cha Dhahabiy, juz/4, uk/35, chapa ya tisa ya Muasasatur-Risaala, Beirut, mwaka 1413.
[8] Rejea kitabu (Al-Kaamil fit-taariikh) imenukuliwa kutoka kwa Ali Munfarid Nadhariy katika kitabu Qissatu Karbala, uk/670, chapa ya sita ya Intishaaraat Suruur, Qum Iran, mwaka 1379.
[9] Rejea gazeti la Risaalat no:6054 la tarhe 16/10/85 Shamsia lililomtafiti Maalik Ashtar na Maisha yake.