advanced Search
KAGUA
8225
Tarehe ya kuingizwa: 2012/05/06
Summary Maswali
nini hukumu ya kupiga sindano ya nguvu au kutia maji ya nguvu (Intravenous injection) mwilini ndani ya Ramadhani?
SWALI
nini hukumu ya kupiga sindano ya nguvu au kutia maji ya lishe (Intravenous injection) mwilini ndani ya mwezi wa Ramadhani? Je kuna ruhusa ya kutumia vitu kama hivyo? Na je vitu hivyo vyaweza kubatilisha saumu? Na kama sindano hizo zitakuwa ni kwa ajili ya dawa je? Pia zaweza kubatilisha saumu?
MUKHTASARI WA JAWABU

Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo:

Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: iwapo sindano hizo zitakuwa ni kwa ajili ya lishe au zitakuwa na aina fulani ya lishe, basi ni bora kua na tahadhari nazo na kujiepusha nazo, lakini zitapokuwa ni kwa ajili ya dawa au kwa ajili ya ganzi, basi hakutokuwa na tatizo kuzitumi sindano hizo.

Fadhil Lankarani (r.a) naye anasema: mwenye saumu anatakiwa kujiepusha na sindano na maji ya kutia nguvu mwilini, lakini hakuna tatizo kupiga sindano za dawa au za ganzi katika hali ya saumu.

Makari Shirazi (Mola amhifadhi) naye anasema: kwa kuchukua hadhari ya kutoharibika funga, ni lazima mtu ajiepushe na sindano za kutia nguvu pamoja na za dawa, pia asitumie maji ya lishe ambayo yanaingizwa kwa mirija maalumu mwilini, lakini hakuna tatizo kutumia sindano za ganzi.

Mwana chuoni Jawadi Tabrizi, Safi Gulpeigani, Nuru Hamadani, Wahidi Kurasani pamoja Sistani wanasema: sindao yeyote ile haiwezi kubatilisha saumu, ewe ni ya kutia nguvu na lishe  au ni kwa ajili ya dawa.[1]

Jawabu kutoka kwa mwanazuoni Ayatullahi Mahdi Hadawiy Tehraniy (Mungu amuhifadhi) ni kama ifuatavyo:

Piga sindano za nguvu (lishe) pamoja na kutia maji ya lishe au ya nguvu mwilini, ni vitu vilivyoko nje ya hukumu ya kula na ya kunywa, ingawaje ni vizuri mtu kujiepusha na aina hiyo ya sindano pamoja na maji ya nguvu au ya lishe.

Kwa ajili ya kupata faida zaidi rejeo zifuatazo ndani ya tovuti hii:

1- funga na utumija wa dawa, swali la 2986 (tovuti: 3479).

2- kutumia spray katika hali ya saumu, swali la 5845 ( tovuti 6063).

 


[1] Taudhihul-Masail Maraaji, ju/1 uk/892 suala la 1576. Ajwibatul- Istiftaat cha Ayatullahi Khameneiy swali la 767. Taudhihul-Masail cha Ayatullahi wahid Khurasaniy, suala la4851.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • Timsahın saxlanılması və digər ölkələrə satışına icazə varmı?
  5967 دیگر آبزیان
  Təqlid olunan müctehidlərin cavabları bunlardır: Həzrət ayətullah Xamnei (Allah qorusun) Əti haram olan heyvanların saxlanılması və onun hətta, bu heyvanların ətlərinin yeyilməsini halal bilənlərə də satılması düzgün deyildir. Amma, aqillər nəzərində halal mənfəətə görə olsa məsələn, ətinin başqa ət yeyən heyvanlar üçün istifadəsi yaxud, dərisinin dəri sənətində ...
 • Vacip olan kaza orucu bozmanın hükmü nedir? Eğer kaza orucu tutan birisi eşiyle birlikte olursa orucu bozulurmu? Lütfen yardımcı olun.
  3726
  Orucu boazan unsurlar hakkında orucu bozan şeyler, soru:6047 (site:6217) adresine müracaat ediniz. Orucu bozan unsurlardan birisi cinsel ilişki olduğu için ramazan orucu veya kaza orucu arasında hüküm farklılığı yoktur. Yani oruç batıl olur. Ancak ramazan orucunun kazasını yerine getiren şahsın kazayı yerine getirmek için fırsatı varsa öğle ...
 • Nini maana ya Feminism?
  12758 Sheria na hukumu
  Neno (Feminism) linatokana na lugha ya Kifaransa ambalo asili yake ya Kilatini ni (Femind), neno hili hutumika katika lugha mbali mbali huku likiwa na maana moja inayomaanisha uke au jinsia ya kike, ijapokuwa neno hili linapotumika kutoka lugha moja kwenda nyengine huonekana kuwa na mabadiliko kidogo ya ...
 • Batasan pakaian bagi perempuan untuk mengerjakan salat
  4934 پوشش
  Batasan wajib menutup aurat bagi perempuan adalah menutup seluruh badan termasuk rambut kecuali wajah (seukuran dengan basuhan ketika berwudhu), kedua telapak tangan dan kedua kaki sampai pergelangannya. Dari sisi ukuran kainnya, maka kain itu harus bisa menutupi badan artinya seukuran dengan badan dan rambutnya tidak kelihatan. ...
 • nini hukumu ya kupiga sindano ya nguvu au kutia maji ya nguvu (Intravenous injection) mwilini ndani ya Ramadhani?
  8225 گوناگون
  Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo: Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: ...
 • je ndani ya hadithi kuna ushahidi wowote unaoelezea kuwa Ramadhani ni siku tahalathini?
  8581 Elimu ya Hadithi
  Kila mwaka wa Hijiria kwa kawaida huwa una miezi kumi na mbili, na masiku ya miezi huwa yanahesabiwa kwa kuonekana kwa mwezi, hii ni kanuni ya mwaka wa Hijiria, ama mwaka Shamsia kwa kawaida masiku yake huwa tayari yameshatambulikana, na suala la kuonekana kwa mwezi si suala ...
 • nini maana ya itikafu
  16713 اعتکاف
  Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
 • Vipi talaka hutimia, maneno gani hutumika kwa ajili ya talaka, na ni mara ngapi?
  8623 طلاق
  Kulingana na madhehebu ya Shia, iwapo mtu atakasirika kupita budi, kiasi ya kwamba akawa ametoa talaka bila ya makusudia au bila ya hiari kwa kutokana na kutawaliwa na hasira kupita budi. Hapo talaka haitakutimia. Ila kama atakuwa amekasirika kupitia budi, ila bado yupo timamu na akawa ametoa ...
 • je kuutangaza mwezi ni jukumu la wanazuoni wote kwa ujumla, au ni jukumu tu la kiongozi (mwanafiqhi / kadhi) mkuu wa dini nchini?
  8246 رؤیت هلال و یوم الشک
  Fani ya Fiqhi iliyo katika nyanja za juu (iliyobobea), huwa inampa mtu uwezo maalumu wa kuzivua na kuziopoa hukumu kuu za kisheria kutoka katika machimbuko yake, ambayo miongoni mwayo ni zile ibara za Qur-ani na Hadithi takatifu, na jambo hilo (kuwa na uwezo wa kuziopoa hukumu) ni ...
 • ni sharti gani sahihi za utumiaji wa vitu au neema zilizomo ulimwenguni?
  8233 دنیا و زینتهای آن
  Uislamu haukuyazingatia mahitajio ya mwanaadamu kwa upande mmoja tu, kama vile zilivyo fanya dini nyengine, kwani dini nyingi ima hugharamika katika kuyazingatia mahitajio ya kiroho peke yake, au mahitajio ya kilimwengu tu. Uislamu umeshika njia ya kati na kati, na mtizamo wa Uislamu ni kwamba: kufaidika na ...

YALIYOSOMWA ZAIDI