advanced Search

HAZINA YA MASWALI(MPANGILIO WA KIMAUDHUI:Sheria na hukumu)

MASWALI KIHOLELA

  • nini hukumu ya kupiga sindano ya nguvu au kutia maji ya nguvu (Intravenous injection) mwilini ndani ya Ramadhani?
    9980 Sheria na hukumu 2012/05/23
    Wanazuoni wamekhitalifiana kuhusiana na suala hilo. Kwa kupata jawabu tosha, ni lazima utuambie kuwa wewe ni mfuasi wa mwanazuoni gani? Ili tuweze kukupa jawabu makini zaidi. Kwa vyovyote vile mitazamo ya baadhi ya wanazuoni wetu ni kama iuatavyo: Bahjat (r.a) na Khameneiy (Mungu amuhifadhi), wanasema: ...
  • je ni wajibu wangu kulipa fidia ya funga zilizonipita kwa kutokana na uzembe wa wazazi wangu?
    7738 Sheria na hukumu 2012/05/23
    Ofisi ya Ayatullahi Sistani (Mungu ameweke) inajibu kwa kusema: Iwapo wewe ulikuwa hujui kuwa saumu ni wajibu, basi lipa tu hizo funga za miaka minane, na hakuna haja ya kuzilipia fidia. Ofisi ya Ayatullahi Makaarim Shiraziy (Mungu amuweke) nayo inajibu ...
  • je ni kweli kuwa Maimamu ni wabora zaidi kuliko hata Mitume?
    15503 Elimu ya zamani ya Akida 2012/05/23
    Suala la Maimamu (a.s) kuwazidi Mitume katika daraja za kielimu, ni suala moja linalo onekana kuzungumziwa sana na Riwaya mbali mbali, na sababu hasa za wao kuwazidi Mitume kielimu, zinatokana na ule uhakika wa nuru ya maumbile yao, kwani uhakika wa nuru yao unatokana na uhakika wa ...
  • kwa mtazamao wa Kiislamu, mwanaadamu ni kiumbe gani?
    11547 Elimu mpya ya Akida 2012/05/26
    Kwa mtazamo wa Qur-ani, mwanaadamu ni kiumbe aliyebeba sifa mbili tofauti za kimaumbile, moja ni ile inayotokana na maumbile aliyopewa tokea mwanzo kutoka kwa Mola wake, nayo ni maumbile ya kiroho, na ya pili inatokana na maumbile ya kiwiliwili alichonacho. Maumbile asili ya kiroho (kifitra), huwa ni ...
  • je kitabu cha tarehe kijulikanacho kwa jina la Taarekhu-Tabari, ni kitabu kinachoaminika?
    9207 تاريخ بزرگان 2012/05/23
    Pale kitabu fulani kinaposemekana kuwa ni chenye kuaminika, huwa haimaanishi kuwa kila kilichomo ndani yake ni sahihi. Kitabu Taarikhut-Tabariy, si chenye kuepukana na usemi huu, bali nacho pia hakikubeba ndani yake yale yalio sahihi tu. La pili ni kwamba: kauli hiyo ulioinukuu kutoka katika kitabu hicho ...
  • ni zipi funga zilizo zisizofaa kwa mtazamo wa imam Shafi, Hanafi na Maalik?
    14402 Sheria na hukumu 2012/05/23
    Masiku yasiyofaa kufunga saumu mbele ya imam Abu Hanifa ni: siku ya idi ndogo na idi kubwa, pia kufunga siku ya mwezi 11, 12 na 13 ya mwezi wa Dhil-hijja, pia kufunga ndani ya idi pili hadi nne za idi ya mfunguo tatu. Funga zisizofaa ...
  • hebu tufafanulieni umuhimu wa Hadhithi Kisaa (Hadithi ya joho)
    12687 Elimu ya Hadithi 2012/05/23
    Hadhithi Kisaa (Hadithi ya joho) ambayo imenukuliwa ndani ya kitabu cha Sheikh Abbas Qummiy kijulikanacho kwa jina la Mafaatiihul-jinaan, ni Hadithi iliyobeba ndani yake ujumbe mzito wenye umuhimu wa aina mbili. Umuhimu wa kwanza ni kule Hadithi kuwa na fungamano la moja kwa moja na suala la ...
  • Vipi mtu anaweza kuwa kipenzi cha Mwenye Ezi Mungu?
    7188 Tabia kimatendo 2019/06/16
    Katika lugha ya Kiarabu, -ambayo ndiyo lugha ya sheria ya Kiislamu- neno (pendo) linatokana na neno "حب". Ambalo lina maana ya kule mtu kuwa na mapenzi na mtu, kitu au jambo fulani. Lakini neno pendo, mapenzi au neno jengine lenye maana kama hii, linapotumika na kunasibishwa ...
  • nini maana ya ucha Mungu?
    19841 Tabia kimtazamo 2012/05/23
    Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
  • nini siri hasa ya Uslamu kuwa ni dini ya mwisho, na nini pingamizi hasa ya bwana Surush juu ya hilo?
    13417 Elimu ya zamani ya Akida 2014/02/12
    Kuzingatia nukta zifuatazo kutaweza kumsaidia msomaji kulitambua vyema suala hili: 1- Hitimisho la utume lina maana ya hitimisho la dini; na hii inamaanisha kuwa hakutokuja mtume mwengine baada Yake (s.a.w.w). Hayo pia utayakuta kwenye Aya ya 40 ya Suratul-Ahzab. 2- Dini ya Kiislamu imeitwa dini ya mwisho ...

YALIYOSOMWA ZAIDI