advanced Search
KAGUA
9116
Tarehe ya kuingizwa: 2010/09/06
Summary Maswali
je kitabu cha tarehe kijulikanacho kwa jina la Taarekhu-Tabari, ni kitabu kinachoaminika?
SWALI
je kitabu Taarikhut-Tabariy ni kitabu chenye kuaminika? Na je ni sawa kama ilivyonukuliwa ndani ya kitabu hicho kuwa: Imamu Hasan na Husein (a.s) walishiriki kwenye vita dhidi ya Iran vilivyotayarishwa na Omar bin Khattaab, na kama suala hili ni la kweli, basi ni kwa nini Ali (a.s) aliwaruhusu wanawe katika vita hvyo? Na Wairani walikuwa na kosa gani kiasi ya kwamba wasimamishiwe dhidi yao na wauwawe kiholela?
MUKHTASARI WA JAWABU
  1. Pale kitabu fulani kinaposemekana kuwa ni chenye kuaminika, huwa haimaanishi kuwa kila kilichomo ndani yake ni sahihi. Kitabu Taarikhut-Tabariy, si chenye kuepukana na usemi huu, bali nacho pia hakikubeba ndani yake yale yalio sahihi tu. La pili ni kwamba: kauli hiyo ulioinukuu kutoka katika kitabu hicho si kauli iliyonukuliwa ndani ya vitabu vya madhehebu ya Shia.
  2. Kuna baadhi ya wapokezi wasiokubaliana na mpokezi wa Riwaya yenye kulinukuu tokeo hilo, wao wanamuona Ali bin Mjahid kuwa si mtu mwenye kuaminika, wapokezi mbali mbali kama vile: Yahya bin Muin, Yahya bin Dhurais pamoja na Ali bin Hasan Hasan-jaaniy, wamesema kuwa mpokezi wa tokeo hilo ni muongo na ni mtuzi mwenye kujitungia Riwaya kutoka mfukoni kwake.
  3. Iwapo Riwaya ya tokeo hilo itakuwa ni sahihi, basi si tatizo kwa Hasan na Husein kushiriki katika vita kama hivyo, na hii ni kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
  • Ingawaje Wao (a.s) walikuwa si wenye kuwafikiana na uongozi wa makhalifa watatu maarufu, lakini hilo halimaanishi kuwa Imamu Ali na wanawe (a.s) pamoja na wafuasi wao walikuwa wakijitenga na matokeo yaliyokuwa yakihusiana na jamii yao, au wao kutofungamana na sheria za kizalendo.
  • Pia iwapo suala hilo litakuwa na ukweli, basi bila shaka kushiriki kwa watu kama vile Imamu Hasan na Husien (a.s) ndani ya vita kama hivyo, kutakuwa ni kwenye kuleta msaada maalumu wenye kulenga nia ya kuwaingiza watu mbali mbali kwenye mila na tamaduni za Kiislamu, pia kuhudhuria kwao kutasaidia sana katika kuwahami wasio stahili kuhujumiwa, au pia kutazuia mauwaji ya kiholela yanayoweza kufanywa na baadhi ya wale wenye tamaa za kidunia, ambao wangeliweza kufanya aina mbali mbali za uhalifu na uporaji.
  • Hivi kuna nukuu gani zenye kuthibitisha kuwa Wairani waliuwawa kupitia Maimamu hao wawili (Hasan na Husein) (a.s)!
JAWABU KWA UFAFANUZI

Kulibainisha suala hili la Kihistoria, kunahitajia mazingatio maalumu yafuatayo:

  1. Kama tulivyofafanua hapo mwazo kuwa: kuaminika na kukubalika kwa kitabu fulani cha Historia au Riwaya, huwa hakumaanishi kuwa kila kilichomo ndani ya kitabu hicho ni sahihi na chenye kukubalika. Kitabu Taarikhut-Tabariy nacho kiko katika hali hiyo hiyo. Kitabu hichi ni miongoni mwa vitabu vyenye kutegemewa, nacho ni miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Sunni, na kitabu hichi ndicho kilicho nukuu ile habari ya kushiriki kwa Imamu Hasan na Husein (a.s) katika vita dhidi ya Iran vilivyo andaliwa na khalifa wa pili. Lakini suala hili halikunukuliwa na kitabu hata kimoja chenye kuaminika miongoni mwa vitabu vya madhehebu ya Shia. Kuto nukuliwa kwa kisa hicho ndani ya vitabu vya madhehebu ya Shia, kunaashiria ile hali ya wanazuoni wa Kishia kuto kubaliana na kisa hicho.
  2. Kuna baadhi ya wapokezi wa Riwaya kama vile: Yahya bin Muin, Yahya bin Dhurais na …, ambao hawakubaliani na mpokezi wa Riwaya hiyo. Yahya bin Muin kuhusiana na mpokezi huyu anasema: mpokezi huyu ni muundaji wa Hadithi na mzushi. Yahya bin Dhurais kuhusiana naye amesema: huyu ni muongo na ni mwenye kujitungia Hadithi mwenyewe tu, na Ali bin Hasan Hasanjaaniy amesema: mimi nilimuuliza Aba Jaa’far Jammaal (Muhammad bin Mehraan) kuhusiana na uhakika wa Ali bin Mujahid, yeye akaniambia kuwa: Ali bin Mujahid ni muongo.[أ‌] Kwa msingi basi gani sisi tuweze kukubaliana na Riwaya ya mtu kama huyu ambaye wapokezi mbali mbali ni wenye kumkanusha?!
  3. Na hata kama suala hili litakuwa ni lenye ukweli ndani yake, hilo halitaweza kuleta madhara yoyote yale yatakayomtia dosari Hasani na Husein (a.s), kwani suala hilo linahitajia kuzingatiwa na kuangaliwa katika mitazamo ifuatayo:
  • Ingawaje Imamu Hasan na Husein walikuwa ni watoto wa Imamu Ali (a.s), ambaye Yeye (a.s) alikuwa ni mtu wa mwanzo asiyekubaliana na utawala wa zama za makhalifa watatu, kwani kwa mtazamo wake (a.s) ni kwamba: tawala za makhalifa hao hazikuwa ni tawala halali, lakini mtazamo wake huo haukumfanya Yeye na wanawe (a.s) pamoja na wafuasi wao kukaa nje ya jamii yao, au pia kuto kuwa na hali ya uzalendo juu ya taifa lao, bali wao walionekana kuishi na wengine ndani ya jamii yao kama vile wengine walivyokuwa wakiishi. Na hakuna tatizo la wao kuonekana kushiriki ndani ya vita kama hivyo, kwani dunia nzima watu wanaelewa kuwa: mtu asiyekubaliana na utawala wa taifa lake, hawezi kulifanya jambo hilo kuwa ndio kisingizio cha kuto fuata sheria za taifa hilo, au pia kutoshirikiana na wenziwe katika masuala ya kizalendo ya taifa lake kwa kupitia kisingizio hicho.
  • Pia kama suala hilo litakuwa ni la kweli, kushiriki kwa Imamu Hasan na Husein (a.s) katika vita hivyo, si jambo la kutisha, kwani wao si wabadhirifu, bali wao ni pozo litakalowapunuga nguvu au kuwazuia wale wabadhirifu kuto wadhulumu watu kiholela, au kuleta mauaji katika uvamizi wao pasi na misingi madhubuti ya sheria za kivita. Na hilo sio geni, kwani hata katika zama zetu za leo, kila kundi la kivita huwa lina watu maalumu wa kushughulikia haki za wanaadamu, nao huwa ni watu maalumu waliopata mafunzo ya kistaarabu yenye madhumuni ya kuwavuta watu kibusara na kuwafanfa wakubaliane na fikra zao zenye malengo ya kuleta mabadiliko maalumu yaliokusudiwa katika uvamizi wao au kuyatetea madai ya uvamizi huo. Ingawaje Imamu Ali (a.s), alikuwa ni mpinzani wa utawala wa zama zile, lakini yeye hakufunga mikono na kuacha jamii ivurugike, bali alikuwa akichukua juhudi tofauti kwa ajili ya kulizimua joto la maharibiko ya kijamii pale joto hilo lilipokuwa likihatarisha maisha na maendeleo ya wanajamii. Na moja linaloweza kuhesabiwa kuwa ni miongoni mwa harakati hizo, ni kule Yeye (a.s) kuwatuma wanawe wawili (Hasan na Husein) (a.s) katika vita hivyo kwa nia ya kuleta uadilifu ndani ya uvamizi huo.
  • Ingawaje kuna Riwaya yenye kuonesha kuwa Wao (a.s) walishiriki katika vita hivyo, lakini hakuna Riwaya hata moja yenye kudai kuwa Wao (a.s) walikuwa ni miongoni mwa wabadhirifu au wauwaji ndani ya vita hivyo. Kwa hiyo hakuna jambo la kutisha litakaloweza kutufanya sisi kuwatia mashakani Hasan na Husein (a.s), na hata ndani ya kitabu Taarikhut-Tabariy, Wao (a.s) hawakutajwa kuwa ni miongoni mwa wauwaji walioshiriki ndani ya dhulma fulani iliofanyika ndani ya uvamizi huo.

Huu ndio mwisho wa uhakiki juu ya suala hili, na hii ndiyo natija tulioweza kuifikia ndani ya uhakiki wetu huu.


[أ‌] Tahdhibul-kamaal cha Al-Mazjiy, juz/21, uk/118 hadi 119, (Maktabatush-shaamila).

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI