advanced Search
KAGUA
4870
Tarehe ya kuingizwa: 2009/09/14
Summary Maswali
je mababu na wana wa Maalik Ashtar walikuwa ni wapenzi na wanaumini wanao uunga mkono uongozi wa Ahlul-Bait (a.s)?
SWALI
je mababu wa Maalik Ashtar walikuwa ni waumini? Na je Maalik Ashtar alikuwa na mtoto? Na kama alikuwa naye, je mwanawe naye alikuwa ni muridi (mpenzi na mfuasi) wa Ahlul-Bait (a.s) au la?
MUKHTASARI WA JAWABU

Kwa kweli hakuna kitabu miongoni mwa vitabu maarufu vya Tarehe vyenye kutegemewa kilichozungumzia na kuthibitisha suala la hali halisi juu ya wazee wa Maalik Ashtar, bali tu kinachofahamika kuhusiana nao, ni kuwa wao ni watu wa makabila ya (Nukha’a) na (Mudh-haj) yalioko huko Yemen, lililothibitika ndani ya Tarehe ni kwamba, makabila haya yalikuwa ni miongoni mwa makabila ya mwanzo yaliyoukubali na kuuamini Uislamu.

Maalik Ashtar alikuwa na watoto wawili wa kiume, mmoja alijulikana kwa jina la Is-haaq na mwengine Ibrahim. Is-haaq alikuwa ni mfuasi wa Imam Husein (a.s) aliyemuunga mkono Imamu Husein (a.s) kwenye mapambano ya Karbala, na hatimae kuuwawa katika mapambano hayo, na Ibrahim naye alikuwa ni mfuasi wa Ahlul-Bait (a.s), naye alishiriki katika mapambano yaliyotekea katika vugu vugu la kutaka kulipiza kisasi cha mauaji ya Imam Husein (a.s), vugu vugu ambalo lilianzishwa na Mukhtari Thaqafiy, huku Ibrahim akiwa ni miongoni mwa makamanda wa kivita ndani ya tokeo hilo, yeye aliifanya kazi yake kwa vizuri pasi na woga, na wengi miongoni mwa majahili waliomdhulumu Husein (a.s) walipata jaza yao ya kifo kupitia mkononi mwa Ibrahim, na mmoja miongoni mwa majahili muhimu alioweza kuwateketeza, ni Ibnu Ziad, ambaye alikuwa ndiye shetani mkuu dhidi ya Imamu Husein (a.s). vitabu vya Tarehe vinaelezea kuwa, Ibrahim alikuwa na watoto watano, nao ni: Nuuman, Maalik, Muhammad, Qasim na Khuulaan. Na miongoni mwa watoto hao watano, wapo watoto wawili ambao walikuwa ni wapokezi wa Hadithi, mmoja wao akiwa ni Muhammad na wa pili akiwa ni Qaasim.

JAWABU KWA UFAFANUZI

Maalik bin Harith bin Abdu-Yaghuth bin Salma bin Rabia bin Harith bin Khuzaima bin Sa’ad bin Maalik bin Nukha’a, anatokana na koo mbili asili zilizo shujaa nazo ni Nukha' na Mudh-haj.[1] Yeye alizaliwa katika zama za kijahili kabla ya kuja kwa Uislamu,[2] ama kuhusiana na namna ya kusilimu kwake yeye mwenyewe au ukoo wake, ni moja ya mambo ambayo hayakufafanuliwa na vitabu vya Tarehe, na wala hakuna Hadithi au mfano wa Hadhithi uliolizungumzia suala hilo.[3] Baadhi ya waandishi wanakadiria kuwa yeye alisilimu pale Imamu Ali (a.s) alipokwenda Yemen kuutangaza Uislamu.[4] Kwani makabila mengi yaliukubali Uislamu na kusilimu makundi kwa makundi, kama vile kabila la Hamdaan, Nukha’a na Mudh-haj.

Katika zama za ukhalifa wa Abu Bakar, ukoo huu asili wa Kiarabu ulishika njia ya Sham (Siria) kisha ukaelekea Iraq kwenye mji maarufu ujulikanao kwa jina la (Kuufa), na hapo ndipo yakawa makazi ya kabila hilo, wao walizaliana na kukusanyika siku baada ya siku, hadi ukoo wao ukakua na kuota mizizi ndani ya mji huo. Kizazi cha maalik kilikua siku baada ya siku, na hatimae kizazi hicho kikazaa koo kubwa zilizojulikana kwa jina la (Banu Maalik), (Banu Ibrahim) n.k. Pia hadi leo kuna koo mbali mbali ambazo nasabu zake zinatokana na Maalik Ashtar, na miongoni mwa koo hizo ni Aalu Kaashiful-Ghitaa na Aalu Radhiy.

Imenukuliwa kutoka kwenye vitabu vya Tarehe kuwa, Maalik alikuwa na watoto wawili waliojulikana kwa majina ya Ibrahim na Is-haaq. Is-haaq alikuwa ni mfuasi mkereketwa wa Imamu Husein (a.s) ambaye alishika upanga katika vita vya Karbala baada tu ya kuuwawa kwa Habib bin Madhahir, na hatimae akauwawa katika vita hivyo.[5] Ibrahim alikuwa ni mtoto shujaa wa Maalik Ashtar, ambaye ni mpenzi na mfuasi shupavu wa Ahlul-Bait (a.s). Yeye alikuwa ni Shia madhubuti aliye makini kiimani na kimatendo, na hakufanana tu na baba yake kiimani na kimatendo, bali pia alifanana naye kimwili pamoja na sura.[6] Muandishi maarufu wa Tarehe ajulikanaye kwa umaarufu wa Dhahabiy, amenukuu kutoka kwa waandishi wa Tarehe wa madhehebu ya Kisunni akisema: “Ibrahim alikuwa ni shujaa kama baba yake aliyebobea sifa njema na alikuwa ni miongoni mwa watu watukufu”.[7] Ibrahim alishiriki mapinduzi muhimu yaliosimamishwa na Mukhtari Thaqafiy kwa nia ya kutaka kulipiza kisasi na kuwapandisha katika kiriri cha sheria  wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyengine katika mauwaji ya Imamu Husein (a.s). Ibrahim waliweza kuwatokomeza maadui wengi wa Ahlul-Bait (a.s) ambao walishiriki katika mauaji ya Karbala, na miongoni mwa wale walioteketea kupitia mkononi mwake, ni Ibnu Zaid ambaye alimteketeza ndani ya siku ya kumi ya mwezi wa Muharram ya mwaka 67 Qamaria.[8] Vitabu vya Tarehe vimenukuu kuwa Ibrahim alikuwa na watoto watano waliojulikana kwa majina yafuatayo: Nuumani, Maalik, Muhammad, Qaasim na Khuulaan. Miongoni mwa watoto hawa, mna wale watoto wawili ambao walikuwa ni wapokezi wa Hadithi, nao ni Muhammd na Qaasim.[9]

Kwa ajili ya utafiti zaidi rejea: kitabu (A’ayani Shia) cha Sayyid Muhsin Amin, juz/2, uk/200, Daarut-Ta’ariif lilmatbuua’at, Beirut Lebanon, mwaka 1406 Qamaria.

 


[1] Dairatul-Maarif Shial- A’amma cha  Muhammad Husein A’alamiyul-Haairiy, juz/16, uk/40, chapa ya pili ya Muasastul-A’alamiy lilmatbuua’at, Beirut, chapa ya mwaka 1413. Pia  kitabu A’ayanush-Shia cha Sayyid Muhsin Al-Amin, juz/9, uk/38, chapa ya Dairatul-Ma’arif lilimatbuua’at, Beirut , chapa ya mwaka 1403. Pia kitabu Maalik Ashtar Khutabihi wa Aaraihi, cha Qeisul-Attaar, uk/13, chapa ya kwanza ya Muasasatul-Fikril-Islamiy Iran ya mwaka 1412.

[2] Rejea kitabu Al-A’alaam cha Khairud-Diin Al-Rarkaliy, juz/5, uk/259, chapa ya kwanza ya Daarul-Ilm, Beirut.

[3] Rejea kitabu Maalik Ashtar cha Sayyid Muhammad Ridha Al-Hakim, uk/33, chapa ya kwanza ya Maktabatul-Haidariyya Qum Iran, ya mwaka 1427.

[4] Rejea kitabu Maalik Ashtar cha Muhammad Muhammadiy Ishtihardiy, uk/19, chapa ya pili ya Intishaaraat Peyam Aazaadiy Tehran, mwaka 1372.

[5] Rejea kitabu Maalik Ashtar cha Muhammad Muhammadiy Ishtihardiy, uk/188.

[6] Dairatul-Maarif Shial- A’amma cha  Muhammad Husein A’alamiyul-Haairiy, juz/2, uk/131.

[7] Seiru A’alaamin-Nubalaa cha Dhahabiy, juz/4, uk/35, chapa ya tisa ya Muasasatur-Risaala, Beirut, mwaka 1413.

[8] Rejea kitabu (Al-Kaamil fit-taariikh) imenukuliwa kutoka kwa Ali Munfarid Nadhariy katika kitabu Qissatu Karbala, uk/670, chapa ya sita ya Intishaaraat Suruur, Qum Iran, mwaka 1379.

[9] Rejea gazeti la Risaalat no:6054 la tarhe 16/10/85 Shamsia lililomtafiti Maalik Ashtar na Maisha yake.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • kwa nini Imamu Husein (a.s) anaitwa Tharu-Llahi (ثار الله)?
  7685 زیارت عاشورا و دیگر زیارات
  Neno Tharu-Llahi (ثار الله) limekuja likiwa na maana mbili: moja ni kwa maana ya damu, na ya pili ni kwa maana ya kulipiza kisasi na kutaka kummwga damu ya muuwaji. Kwa hiyo maana ya mwanzo inapotumika kwa ajili ya kumuita Yeye (a.s) Tharu-Llahi (
 • je kitabu cha tarehe kijulikanacho kwa jina la Taarekhu-Tabari, ni kitabu kinachoaminika?
  5792 امام حسین قبل از امامت
  Pale kitabu fulani kinaposemekana kuwa ni chenye kuaminika, huwa haimaanishi kuwa kila kilichomo ndani yake ni sahihi. Kitabu Taarikhut-Tabariy, si chenye kuepukana na usemi huu, bali nacho pia hakikubeba ndani yake yale yalio sahihi tu. La pili ni kwamba: kauli hiyo ulioinukuu kutoka katika kitabu hicho ...
 • je majina ya watu watano watukufu yametajwa ndani ya Taurati na Injili?
  9340 اهل بیت و ذوی القربی
  Kwa mujibu wa nukuu za baadhi ya Hadithi ni kwamba, majina ya matano ya Aali Abaa (a.s), yaani Aali wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambao ni: Ali, Fatima,Hasan na Husein, yametajwa ndani ya Taurati na Injili. Pia suala hilo linaonekana kuashiriwa ndani ya ile Hadithi yenye kunukuu majadilianao ...
 • je mwenye saumu anaruhusiwa kukoga janaba?
  14749 جنابت
  Mtu anaweza kupatwa na janaba katika hali mbili: ima itakuwa ni kabla ya adhana ya asubuhi au baada ya adhana ya asubuhi, lakini janaba tunalolizungumzia hapo ni lile janaba la dharura, kama vile dharura ya kuota, siyo la kupiga ponyeto au kujamii. Kukoga janaba kabla ...
 • kwa mtazamao wa Kiislamu, mwanaadamu ni kiumbe gani?
  7673 Elimu mpya ya Akida
  Kwa mtazamo wa Qur-ani, mwanaadamu ni kiumbe aliyebeba sifa mbili tofauti za kimaumbile, moja ni ile inayotokana na maumbile aliyopewa tokea mwanzo kutoka kwa Mola wake, nayo ni maumbile ya kiroho, na ya pili inatokana na maumbile ya kiwiliwili alichonacho. Maumbile asili ya kiroho (kifitra), huwa ni ...
 • nini maana ya neno (dini)? Au dini hasa ni kitu gani?
  32307 Falsafa ya Dini
  Wamagharibi wametumia ibara mbali mbali ili kupata maana muwafaka inayowafikiana na neno (dini), na neno (dini) ndani ya Qur-ani limetumika huku likibeba maana mbili tofauti, nazo ni kama ifuatavyo: 1- dini ni aina yeyote ile ya itikadi yenye kulenga nguvu maalumu za ghaibu zinazoaminiwa na ...
 • kwa nini tuwe wakalidi (wafuasi)?
  4382 تقلیدچیست؟
  Ruhusa ya kumfuata ulamaa maalumu katika matendo ya ibada za kila siku, inatakiwa kutolewa na akili ya mtu mwenyewe. Na wala ruhusa hiyo haingojewi kutoka kwa Maulamaa, huku kila mmoja akielewa umuhimu wa suala hili ndani ya maisha yake ya kila siku. Katika hali yakawaida, ...
 • Vipi mtu anaweza kuwa kipenzi cha Mwenye Ezi Mungu?
  999 Tabia kimatendo
  Katika lugha ya Kiarabu, -ambayo ndiyo lugha ya sheria ya Kiislamu- neno (pendo) linatokana na neno "حب". Ambalo lina maana ya kule mtu kuwa na mapenzi na mtu, kitu au jambo fulani. Lakini neno pendo, mapenzi au neno jengine lenye maana kama hii, linapotumika na kunasibishwa ...
 • tafadhalini tupeni ufafanuzi kuhusu mapokezi na maandiko ya Ziara ya siku ya Ashura.
  6464 زیارت عاشورا و دیگر زیارات
  Rejeo mama na asili hasa zinazo aminika ambazo zimeyanukuu maandiko ya Sala na salamu (Ziara) za siku ya Ashura ni vitabu viwili, navyo ni: kitabu Kaamiluz-ziaaraat cha Jaa'far bin Muhammad bin Quulewaihi Qummiy, ambaye amefariki mwaka 348 Hijiria, na cha pili ni kitabu kiitwacho Misbaahul-mujtahid cha ...
 • Shakhsiya yake ilikuwa vipi ?mtazamo wa Ahlul bait kuhusiana na yeye.Riwaya zilizonukuluwa kwake zina hukumu gani?
  1115 تاريخ بزرگان
  Umayri bni Maliki ni katika wajukuu wa khazraji aliyejulikana sana kwa vinyongo,ni katika sahaba wa mtume,[saww]yeye nikatika kabila la watu wa khazraj na aliishi Madina, alisilimu baada ya kupita miezi kadhaa ya mtume kufika Madinah Abu dardaii aliitikadi ubora wa imamAli[as] dhidi ya Muawiyah.Alifatana na Abu Huraira ...

YALIYOSOMWA ZAIDI