advanced Search
KAGUA
10072
Tarehe ya kuingizwa: 2012/05/06
Summary Maswali
ni sharti gani sahihi za utumiaji wa vitu au neema zilizomo ulimwenguni?
SWALI
ni zipi sharti sahihi za utumiaji wa vile vilivyomo ulimwenguni?
MUKHTASARI WA JAWABU

Uislamu haukuyazingatia mahitajio ya mwanaadamu kwa upande mmoja tu, kama vile zilivyo fanya dini nyengine, kwani dini nyingi ima hugharamika katika kuyazingatia mahitajio ya kiroho peke yake, au mahitajio ya kilimwengu tu. Uislamu umeshika njia ya kati na kati, na mtizamo wa Uislamu ni kwamba: kufaidika na neema mbali mbali za Mwenye Ezi Mungu zilizomo ulimwenguni humu kupitia njia sahihi na salama, si tu jambo hilo  ni lenye kuruhusiwa na si lenye kuhisabiwa kuwa ni miongoni mambo yanayo rudisha nyuma maendeleo ya kiroho, bali jambo hilo linazingatiwa kuwa ni miongoni mwa mambo yanayo saidia kumpa mwanaadamu maendeleo ya kiroho na kumuelekeza katika maisha bora yenye furaha.

JAWABU KWA UFAFANUZI

Dini na madhehebu mbali mbali zilizoshika hatamu kataika jamii mbali mbali za wanaadamu, hutumia njia na mifumo mbali mbali katika kutoa dhamana ya maisha bora kwa wanajamii wake.

Zile taasisi za kidini au kijamii zisizoshikamana na mambo ya kiroho (materialism), huwa hazitilii sana maanani masuala ya kiroho au pia huwa hawa haziyaamini kabisa mambo hayo wala kuyapa thamani yoyote, kwa hiyo wao huamini kuwa maendeleo bora ya mwanaadamu hupatikana na hutukuka kwa kadri ya yeye atakavyoweza kufaidika zaidi na manufaa ya kidunia pamoja na starehe zilizomo ndani yake. Na kwa upande wa pili kuna zile taasisi za kidini na kijamii zinazoamini kuwa: maendeleo ya mwanaadau yatapatikana iwapo yeye ataweza kuepukana au kujitenga na mambo ya kidunia, kwani taasisi hizo za kidini au dini hizo zinaamini kuwa: kushikamana na mambo ya kiroho ndiko kunako muezesha mwanaadamu kuyafikia malengo yake ya maisha bora yenye uhuru kamili, jambo ambalo halitaweza kukamilika bila ya yeye kujitenga kisawa sawa na starehe au manufaa ya kidunia. Kila moja kati ya mitazaomo ya dini hizo, huchipuka na kustawi kutokana fikra maalumu juu ya kumtambua mwanaadamu pamoja na ulimwengo na malengo yake, au malengo ya kuwepo kwa vitu viwili hivi pamoja na fungamano lililopo baina ya mwanaadamu na ulimwengu aishiwo ndani yake.

 

Hapa sisi tunaweza kusema kuwa: kule baadhi ya jamii mbali mbali hasa za Kimagharibi, kushikamana kiswa sawa na starehe za kidunia bila ya kuzingatia mipaka maalumu katika matumizi ya starehe hizo, ndiko kulipopelekea baadhi ya dini au taasisi za kijamii zenye kushikamana na dini, kuwa na siasa kali katika kupingana na starehe pamoja na kufaidika na manufaa mbali mbali ya kidunia, hadi siasa kali hizo zikaelekea katika kuharamisha aina zote zile za matumizi ya starehe za kidunia, bila ya kuzingatia mahitajio ya wanaadamu katika suala hilo.

 

Uislamu haukuyaweka mbali maendeleo ya kiroho na kuyatenganisha na manufaa au starehe maalumu za kidunia ambazo ni moja kati ya neema za Mola Mtukufu kwa ajili ya waja wake, kujitenga na starehe halali za dunia katika mtazamo wa Kiislamu, ni kujidhulumu na ni moja kati ya yale yanayosababisha jamii kurudi nyuma kimaendeleo, na hilo ndilo lililoufanya Uislamu kukataza watu kujitenga moja kwa moja na jamii zao na kujiharamishia manufaa halali ya kidunia (Monasticism). Iamamu Sadiq (a.s) kuhusiana na suala hilo anasema: (Mola Mtakatifu Amemteremsiha Muhammad (s.a.w.w) zile sheria zote alizopewa nabii Nuhu, nabii Musa na nabii Isa (a.s) …sheria ambazo ni nyepesi zenye mfumo safi uendao sawa na maumbile halisi ya mwanaadamu yalivyo, sheria hizo haziruhusu watu kujitenga na jamii pamoja na kujidhulumu na kuto faidika na neema za Mola wao (Monasticism), bali dini hii imehalalisha yaliyo masafi na kuharamisha machafu, dini hii imekuja kuwatua watu mizigo iliyo waelemea juu yao na kuifungua minyororo  ilioko kwenye shingo zao)[1].

Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na watetezi halisi wa dini hii, walikuwa wakiwaonya watu wasishikamane na dini na kuisahau dunia yao au kuyapa mgongo maisha ya kidunia.

Siku moja mmoja kati ya wafuasi wa Amiril-Muuminiina Ali (a.s), alikwenda kwa Ali (a.s) na kumshitakia kisa cha nduguye ambaye alikuwa ameshikama na dini huku yeye akijitengana kisawa sawa na maisha ya kidunia pamoja na starehe halali zilizomo ndani ya dunia hii, Ali (a.s) alimjibu mfuasi huyu kwa kumwambia:  nenda kamuite huyo nduguyo. Baada ya nduguye aliye julikana kwa jina la Aasim kuwasili, Ali (a.s) alimkabili kwa ghadhabu na hasira huku akimwambia: ole wako ewe Aasim wewe unaelewa vyema kuwa Mola wako amekuhalalishia neema halali zilizomo duniani humu, lakini wewe unaona ni bora kijitenga nazo! Wewe si chochote si lolote mbele ya Mola wako Mtukufu, iweje basi uwe ni mwenye kujiharamishia neema za Mola wako, hivi wewe ni mjuzi zaidi Yake? Hivi wewe huihurumii familia yako? Je wewe unadhani kuwa Mola wako amekuhalalishia yalio halali kwa sababu ya Yeye kuwa na chuki na wewe!?[2].

 

Lazima sisi tufahamu kuwa dini haikatazi watu kunufaika na neema halali zilizomo duniani humu, bali kinachokatazwa ni kule kuivamia dunia na kujigubika nayo, jambo ambalo huwa ndiyo sababu itakayomfanya mwanaadamu kughafilika na kumsahaulisha wadhifa wake juu ya viumbe wengine au wadhifa wake mbele ya Mola wake na hatimae kumpoteza na kumueleza katika maangamio, jambo ambalo humpelekea yeye kuyasahau maisha ya Akhera, kujivuna, kutakabari, kufanya israfu (matumizi mabaya), kuto kuwa na shukurani n.k. lakini pale mja atakapo ihisabu dunia kuwa ni kama ngazi ya kuielekea Akhera yake pamoja na kujikaribisha na Mola wake, hapo dunia na neema za duniani hazitokuwa ni tatizo au kikwazo juu yake, na kwa mtindo kama huu dunia haitohisabiwa kuwa ni kitu kibaya, na kuna Riwaya chungu nzima zenye kuufafanua ukweli huu, na miongoni mwazo ni Riwaya mbili zifuatazo:

  1. Kulikuwa na mtu mmoja aliyeishutumu na kuiponda dunia mbele ya Amiirul-Muuminiina Ali (a.s), Ali (a.s) alimkabili mtu huyo kwa jawabu zifuatazo: elewa kuwa dunia ni nyumba ya ukweli kwa wasemao ukweli, ni nyumba ya afya kwa wale wenye kuitambua dunia vilivyo, ni nyumba ya kujazo na kufungasha kwa wale wenye kutaka kwa kufunga na kujaza mizigo yao na pia dunia ni nyumba yenye hekima kwa wenye kutaka kujifunza hekima. Dunia hii ndio masujudio ya wapenzi wa Mola, ni msikiti wa Malaika wa Mwenye Ezi Mungu, ni mashukio ya Wahyi na ni soko la biashara kwa wapenzi wa Mola wenye kuzitafuta rehema za Mola wao ndani ya soko hilo na kujipatia faida ya Pepo ndani yake.[3]
  2. Ibnu Yaa’fuur amesema kuwa: nilimuambia Imamu Sadiq (a.s) ya kuwa, sisi ni miongoni mwa wenye kuipenda dunia, Yeye (a.s) akanijibu: wewe una malengo gani katika kuipenda kwako dunia hii? Nikamjibu: kwa ajili ya kuowa, kwenda hija, kuwasaidia jamaa zangu, na pia kuwasaidia ndugu zangu na kuwapa watu sadaka, Imamu (a.s) akanijibu kwa kusema: hayo yote uliyo yataja hayamo katika masuala ya kidunia, kwani hizo ni amali zenye kufungamana moja kwa moja na makazi ya Akhera.

Tunamuomba Mola atuwafikishe kufanya mambo ya kheri, aamin.

Mwisho wa makala.

 

 


[1] Al-Kafi cha Muhammad bin Yaa’quub Koleiniy, juz/8, uk/22, chapa ya Darul-Kutubil-Islamiyya, Tehran, mwaka 1365 Shamsia.

[2] Rejea rejeo lililopita, juz/1, uk/410.

[3] Nahjul-Balagha, uk/492, hekima ya 131, chapa ya Darul-Hijra, Qum.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI