advanced Search
KAGUA
15524
Tarehe ya kuingizwa: 2012/04/07
Summary Maswali
hadi kufia leo, ni watu gani walio weza kusimama mbele ya shetani, na walitumia njia gani katika kupambana naye?
SWALI
shetani na jeshi lake la kijini tokea zamani wameamua kukabiliana na wacha Mungu na kupambana nao kupitia aina mbali mbali za mashambulizi, hufanya hivyo kwa ajili ya kuwalazimisha wacha Mungu kumkufuru Mola wao. Je hadi leo kuna watu wowote wale walioweza kusimama kidete na kupingana na mashetani hao, na kama jawabu itakuwa dio, basi ni njia gani walizozitumia watu hao katika kupambana na mashetani hao? Naomba jawabu muwafaka. Ahsanteni sana kwa juhudi zenu.
MUKHTASARI WA JAWABU

Kwa mtazamo wa Qur-ani ni kwamba: shetani hana uwezo wa kuwamiliki na kuwadhibiti wacha Mungu wenye ikhlasi na Mola wao.

Wacha Mungu wenye ikhlasi, ni wale walio ifikia daraja maalumu ya ucha Mungu, jambo ambalo huwa ndiyo ngao iwalindayo kutokana na shetani. Kupambana na shetani kunahitajia zana na silaha maalumu, na kupitia silaha hizo mja huwa ndiye mshindi atakayemtupa chini shetani ndani ya uwanja wa mieleka na kuibuka na medali ya ushindi. Baadhi ya silaha hizo za kupambana na shetani, ni kama ifuatavyo:

  1. Imani (itikadi madhubuti): Qur-ani takatifu imeihesabu imani kuwa ndio silaha msingi itakayomfanya shetani ashindwe kumdhibiti mja.
  2. Kutawakali (kumtegemea Mola): kumtegemea Mola ni silaha nyengine imuwezeshayo mja kumshinda adui yake (shetani), pamoja na jeshi lake.
  3. Kujilinda kupitia Mola Muweza: kumuweka Mola kuwa Ndiye ngao, ni njia muhimu ya kumshinda shetani.
  4. Kumtaja Mola (au kumkumbuka Mola kila wakati): kumkumbuka Mola wakati wote, ni jambo linalomfanya mja aepukana na wasi wasi utokanao na shetani, wasi wasi ambao huwa ndio njia kuu ya shetani.
  5. Kuwa na taqwa (ucha Mungu): ucha Mungu ni nguzo inayoyafungua macho ya moyo, macho ambayo humfanya mja auone vyema wasi wasi wa shetani na kuepukana nao.
JAWABU KWA UFAFANUZI

Kwa mtazamo wa Qur-ani ni kwamba: shetani huwa ni mtawala ndani ya nyoyo za wale wenye maradhi ndani ya nyoyo zao, lakini yeye (shetani) hana mamlaka yoyote yale katika kuwadhibiti wacha Mungu, na ukweli huu umethibitishwa na shetani mwenyewe, kama vile Qur-ani inavyo tuthibitishia hilo kwa kusema:

"قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ ‏‏ إِلاَّ عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ"

Maana yake ni kwamba: (Akasema (shetani) nami ninaapa kwa Utukufu wako kwamba, mimi nitawapotosha wanaadamu wote, isipokuwa tu wale waja wako ambao ni miongoni mwa wacha Mungu (wenye ikhlasi).)[1]

Pia tunaweza kuufahamu ukweli huu kupitia Aya isemayo:

" إِنَّ عِبادي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطانٌ إِلاَّ مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغاوينَ "

Maana yake ni kama ifuatavyo: (Kwa hakika waja wangu huna uwezo nao wa kuwamiliki na kuwadhibiti, ila wale watakaokufuata na kukutii miongoni mwa wale waliopotoka (hao ndio utakaowadhibiti).)[2]

Kwa jinsi ya maelezo ya Aya hizi ni kwamba: kundi pekee liwezalo kuepukana na uvamizi wa shetani, ni lile kundi la wacha Mungu (wenye ikhlasi), na ukweli huu umesemwa na shetani mwenyewe, na pia Mola Mtukufu ameutilia mkazo ukweli huo pale aliposema:

"إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ"

Maana yake ni kwamba: (Kwa hakika wewe (shetani) huna mamlaka  wala uwezo wa kuwadhibiti waja wangu).

Njia za kukabiliana na shetani

Wenye ikhlasi ni wale walioifikia daraja maalamu miongoni mwa daraja za ucha Mungu, daraja ambayo huwa ndio ukuta na ngao imzuiayo shetani kupenya na kuwahujumu waja hao. Kukabiliana na shetani kunahitajia nyenzo na njia maalumu, nyenzo ambazo humuwezesha mja kupambana na shetani na hatimaye kuibuka na ushindi kutoka katika uwanja wa mieleka baina ya waja na mashetani. Sisi hapa tutatumia fursa hii katika kuelezea baadhi ya njia na nyenzo za kukabiliana na shetani kama ifuatavyo:

  1. Imani na itikadi madhubuti ni moja kati ya misingi mikuu iliyozingatiwa na Qur-ani ikiwa ni kama silaha madhubuti ya kupambana na shetani. Qur-ani ikizungumzia ukweli huu imesema:

‏"إِنَّهُ لَيْسَ لَهُ سُلْطَانٌ عَلَى الَّذِينَ آمَنُواْ وََ..."

Maana yake ni kwamba: (Kwa hakika shetani hana mamlaka wala nguvu za kuwadhibiti waumini…).[3]

  1. Njia na nyenzo nyengine ya kukabiliana na shetani na jeshi lake, ni kumtegemea Mola Mlezi. Mwenye Ezi Mungu kuhusiana na hili amesema:

" إِنَّهُ لَيْسَ لَهُ سُلْطَانٌ عَلَى الَّذِينَ ... وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ "

Maana yake ni kwamba (Kwa hakika yeye (shetani) hana mamlaka juu ya wale… ambao ni wenye kumtegemea Mola wao.)[4]

Kumuamini Mola pamoja na Aya zake ni ngome bora inayomfanya mja aepukane na utawala wa shetani, na kwa wale waliojikinga kupitia ngao ya imani huku wakimtegemea Mola wao katika kujilinda kwao na shetani, hao hawatotiwa mkononi na kutawaliwa na shetani. Kwani nguvu za utawala wa shetani huwa zinawadhibiti na kuwatawala wale tu waliokubaliana na utawala huo huku wakimshirikisha Mola wao. Na kuhusiana na jambo hili Qur-ani takatifu inasema:

"إِنَّمَا سُلْطَانُهُ عَلَى الَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُ وَالَّذِينَ هُم بِهِ مُشْرِكُونَ"

Maana yake ni kwamba: (Kwa hakika mamlaka ya utawala wake (shetani) huwa juu ya wale wenye kumfanya yeye kuwa ndiye mtawala wao na wale wenye kumshirikisha Mola wao).[5]

3-    Kujilinda kumpitia Mola Mtakatifu: kujilinda tunakokumaanisha hapa, ni kutaka msaada kutoka kwa Mola Mtukufu. Kumuomba Mola msaada kunaweza kukawa kwa ajili ya kutaka kuepukana na moja kati ya aina mbili za shari, afu zote mbili kwa pamoja, aina ya kwanza ni kumuomba Yeye msaada kutokana na shari zinazotokana na hali halisi ya maumbile ya ulimwengu yanavyo kwenda, na ya pili ni kumuomba Yeye msaada kutokana na wasi wasi wa shetani pamoja na shari za walimwengu. Bila shaka ndani ya ulimwengu huu kuna aina mbali mbali za motokeo ya hatari, matokeo ambayo huwa ima yanatokana na nyenendo za walimwengu katika kuleta ufisadi ndani ya ulimwengu huu, au kwa wakati mwengine huwa yanatokana na maumbile ya dunia yalivyo. Na kwa upande wa pili pia huwa kuna maotokeo ya hatari na shari maalumu zinazosababishwa na nafsi za wanaadamu au majini. Mola Mtukufu akimtahadharisha Mjumbe wake (s.a.w.w) pamoja na kututahadharisha sisi kwa ujumla, amesema:

" وَ إِمَّا يَنْزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّهِ إِنَّهُ سَميعٌ عَليم‏"

Maana yake ni kwamba: (Na iwapo utapata aina fulani ya wasi wasi utokao kwa shetani, basi jilinde na Mola wako, kwani Yeye ni mwenye kusikia na ni mjuzi).[6]

Msingi wa imani ni wenye kumfanya mja amtegemee Mola wake katika kutafuta kheri na manufaa yake, na kule mja kuaza kazi au matendo na ibada zake za kila siku kwa jina la Mola wake, ni alama na dalili tosha zinazoonesha tegemeo lake kwa Mola wake, kwani kila mmoja wetu ni mwenye kuelewa kwamba: hakuna yeyote yule awezae kumnufaisha au kumdhuru mja, bila ya kupata idhini kutoka kwa Mola wake.

4- kumkumbuka Mola katika wakati wote: kuwa pamoja na Mola kila wakati, huwa kunamfanya mja awe na uoni wenye kumuepusha yeye na wasi wasi wa shetani, kwani kumkumbuka mola kila wakati ni ngao imara ya kumtenga mja na shetani.[7]

Imamu Saadiq (a.s) amesema: (shetani hana uwezo wa kumtia mtu wasi wasi, isipokuwa pale mja huyo atakapoghafilika na Mola wake).[8] Imau Ali (a.s) naye amesema:

"ذکرالله مطردة الشیطان."

Maana yake ni kwamba: (Kumkumbuka Mola (kumtaja Mola) ni jambo lenye kumkimbiza shetani).[9]

5- Ucha Mungu: kuifikia daraja ya ucha Mungu na kuilinda isitokomee, ni jambo lenye kumfungua mtu macho ya moyo wake, na iwapo moyo wa mtu fulani utakuwa macho, basi mtu huyo hato hujumiwa na wasi wasi wa shetana, Mola wetu anasema:

" إِنَّ الَّذينَ اتَّقَوْا إِذا مَسَّهُمْ طائِفٌ مِنَ الشَّيْطانِ تَذَكَّرُوا فَإِذا هُمْ مُبْصِرُون‏"

Maana yake ni kwamba: (Kwa hakika wale wacha Mungu pale wanapohujumiwa na wasi wasi wa shetani, huwa wanamkumbuka Mola pamoja na hatari ya siku ya malipo, na papo hapo hugutuka na kuuona uhakika wa mambo yalivyo).[10]

Neno (طائِفٌ) katika Aya iliyopita, lina maana ya kuzunguka, hii ina maana ya kwamba: wasi wasi wa shetani huwa unamzunguka mtu kutoka kila pembe kwa ajili ya kutaka kumghilibu, huku wasi wasi huu ukisubiri aina fulani ya udhaifu ili uweze kuitumia fursa hiyo kwa ajili ya kumpotosha mwanaadamu huyo.

Lakini iwapo mja atakuwa ana chumo na rasili mali ya taqwa (ucha Mungu), hapo shetani hatoweza kupata upenyo wa kumuingia na kumhujumu mja huyo.

Pia njia ya kupambana na shetani, ni kule mja kufanya jitihada za kukaa na watu wema huku yeye akichukua jitihada za kutenda mema na kutengana na waovu pamoja na maovu yao.

Natija ya utafiti

Kuwa na itikadi madhubuti, ni ngao bora kwa mja yenye kumuepusha yeye kutenda maovu. Vile vlie kumtafakari Mola pamoja na uwezo wake, kunaweza kumpa mtu natija ya kuikuza na kuipa nguvu nafsi yake kwa ajili ya kupambana na shetani. Pamoja na hayo, kuikuza imani na kumtegemea Mola pamoja na kumkumbuka Mola katika wakati wote, ni mambo muhimu ambayo hujenga nguvu madhubuti za kukabiliana na shetani, lakini pia mja asisahau kujilinda na kutaka msaada kutoka kwa Mola wake, pale anapokutana na mambo machafu, na bado sis tusisahau pia kuomba msaada kutoka kwa wanachuoni na mawalii wa Mola kwa ajili ya kujilinda na shetani pamoja na jeshi lake.

Tunamshukuru muulizaji wetu kwa swali lake hili muhimu, kwani yeye amekuwa ndiyo sababu ya kuandikwa kwa makala hii.

Ahsanteni sana, Mungu akubarikini pamoja nasi, aamin.

 


[1] Suratul-Israa, Aya ya 65.

[2] Suratu Hijri, Aya ya 42.

[3] Suratun-Nahlli, Aya ya 99.

[4] Rejea rejeo lililopita.

[5] Rejea rejeo lililopita, Aya ya 100.

[6] Suratul-Aa’raafi, Aya ya 200, na Fussilat, Aya ya 36.

[7] Rejea Auratul-Aa’raafi, Aya ya 201.

[8] Mustadrikul-Wasaaili, cha Muhaddithu Nuuriy juz/1, uk/178, chapa ya Aalul-Bait, Qum, mwaka 1408 Hijiria. Bihaarul-Anwaaru, cha Muhammad Baaqir Majlisiy, juz/72, uk/124, chapa ya Al-Wafaa, Beirut, mwaka 1404 Hijiria.

[9] Ghurarul-Hikami-wa Durarul-Kalimi, cha Abdul-Waahid Amadiy Tamiimiy, uk/188, chapa ya Maktabul-Ii’laamil-Islaamiy, Qum, mwaka 1366 Shamsia.

[10] Suratul-Aa’raafi, Aya ya 201.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

  • Vipi mtu anaweza kuwa kipenzi cha Mwenye Ezi Mungu?
    8835 Tabia kimatendo 2019/06/16
    Katika lugha ya Kiarabu, -ambayo ndiyo lugha ya sheria ya Kiislamu- neno (pendo) linatokana na neno "حب". Ambalo lina maana ya kule mtu kuwa na mapenzi na mtu, kitu au jambo fulani. Lakini neno pendo, mapenzi au neno jengine lenye maana kama hii, linapotumika na kunasibishwa ...
  • je mtu asiwajibikiwa kufunga (asiyefunga) ana ulazima wa kutoa zakatul-fitri?
    11954 زکات فطره 2012/05/23
    Mtu atakaeingiliwa na usiku wa Idil-fitri, huku akiwa ni baleghe na mwenye akili timamu, naye akiwa si mtumwa wa mtu wala si fakiri, mtu huyo atawajibika kutoa zakatul-fitri kwa ajili yake na kwa ajili ya wale wote anaowahudumia, na kiwango cha kila mmoja ni kiasi cha kilo ...
  • maadili mema yana nafasi gani kwenye uwanja wa mazoezi?
    12966 Tabia kimatendo 2012/05/23
    Uisalmu ni dini kamili iliyokusanya ndani yake mfumo kamili na salama wenye kutoa muelekeo wa kiutendaji kuhusiana na kipengele kimoja kimoja miongoni mwa vile vipengele vinavyo husiana na maisha ya mwanaadamu. Uislamu haukuliweka nyuma suala la afya ya mwili wa kila mmoja wetu. Kwa hiyo Uislamu ni ...
  • kwa nini Uislamu unaamuru kuwanyonga wanaoritadi? Je hilo haliendani kinyume na uhuru wa kila mmoja kuabudu anacho kitaka?
    22870 حدود، قصاص و دیات 2012/05/23
    Kuritadi ni kitendo cha wazi kabisa cha kutoka katika dini, na mara nyigi tendo hilo hutumika kama ni nyenzo ya kuwadhoofisha wengine kiimani na kuwafanya waache dini yao, na hatimae kuwatoa na kuwaweka nje ya dini. Wanaohukumiwa hukumu ya kuritadi, ni wale wanaolidhihirisha tendo hilo kwa wengine, ...
  • nini maana ya itikafu
    21325 اعتکاف 2012/05/23
    Neno (itikafu) kilugha, huwa lina maana ya kule mtu kukaa na kubaki katika sehemu au pahala maalumu, huku akiwa ameshikamana na jambo maalumu ndani ya mahala hapo, lakini neno hili kitaalamu (kwenye fani ya sheria za Kiislam) linamaanisha kule mtu kukaa katika sehemu takatifu kwa ajili ya ...
  • je kitabu cha tarehe kijulikanacho kwa jina la Taarekhu-Tabari, ni kitabu kinachoaminika?
    10553 امام حسین قبل از امامت 2012/05/23
    Pale kitabu fulani kinaposemekana kuwa ni chenye kuaminika, huwa haimaanishi kuwa kila kilichomo ndani yake ni sahihi. Kitabu Taarikhut-Tabariy, si chenye kuepukana na usemi huu, bali nacho pia hakikubeba ndani yake yale yalio sahihi tu. La pili ni kwamba: kauli hiyo ulioinukuu kutoka katika kitabu hicho ...
  • je ni kweli kuwa Maimamu ni wabora zaidi kuliko hata Mitume?
    16934 دانش، مقام و توانایی های معصومان 2012/05/23
    Suala la Maimamu (a.s) kuwazidi Mitume katika daraja za kielimu, ni suala moja linalo onekana kuzungumziwa sana na Riwaya mbali mbali, na sababu hasa za wao kuwazidi Mitume kielimu, zinatokana na ule uhakika wa nuru ya maumbile yao, kwani uhakika wa nuru yao unatokana na uhakika wa ...
  • nini hukumu ya kufuga njiwa ndani ya sheria za Kiislamu? Na nini msingi hasa wa hukumu hiyo?
    26426 نگهداری و شکار حیوانات 2012/06/17
    Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
  • Je ni kweli kuwa Imamu Husein (a.s) aliwahi kuwa na binti mwenye umri wa miaka mitatu au mine, aliyejulikana kwa jina la Ruqayya au Sukaina anaye semekana kuwa alifariki dunia huko Damascus?
    11645 اهل بیت و یاران 2012/05/23
    Ingawaje wengi miongoni mwa waandishi wa Historia hawakukinukuu kisa cha kuwepo kwa mtoto huyo wa kike wa Imamu Husein (a.s) mwenye umri wa kiasi cha miaka mitatu au mine, aliyejulikana kwa jina la Ruqayya au Fatimatu Sughra na baadhi ya wakati akijulikana kwa majina yasiokuwa hayo, lakini ...
  • je dini na siasa ni vyenye kuendana au vyapingana?
    14099 Elimu mpya ya Akida 2012/05/23
    Dini ni chombo maalumu kilichokuja kumkomboa mwanaadamu na kumuongoza katika njia ya mafanikio, hivyo basi ni jambo lisiloingia akilini kuwa chombo hichi kiwe ni chenye kulipa mgongo jambo muhimu linalohitajika ndani ya jamii mbali mbali, kama vile suala la usimamishaji wa serikali. Na kwa upande mwengine ni ...

YALIYOSOMWA ZAIDI