advanced Search
KAGUA
4652
Tarehe ya kuingizwa: 2009/09/14
Summary Maswali
je mababu na wana wa Maalik Ashtar walikuwa ni wapenzi na wanaumini wanao uunga mkono uongozi wa Ahlul-Bait (a.s)?
SWALI
je mababu wa Maalik Ashtar walikuwa ni waumini? Na je Maalik Ashtar alikuwa na mtoto? Na kama alikuwa naye, je mwanawe naye alikuwa ni muridi (mpenzi na mfuasi) wa Ahlul-Bait (a.s) au la?
MUKHTASARI WA JAWABU

Kwa kweli hakuna kitabu miongoni mwa vitabu maarufu vya Tarehe vyenye kutegemewa kilichozungumzia na kuthibitisha suala la hali halisi juu ya wazee wa Maalik Ashtar, bali tu kinachofahamika kuhusiana nao, ni kuwa wao ni watu wa makabila ya (Nukha’a) na (Mudh-haj) yalioko huko Yemen, lililothibitika ndani ya Tarehe ni kwamba, makabila haya yalikuwa ni miongoni mwa makabila ya mwanzo yaliyoukubali na kuuamini Uislamu.

Maalik Ashtar alikuwa na watoto wawili wa kiume, mmoja alijulikana kwa jina la Is-haaq na mwengine Ibrahim. Is-haaq alikuwa ni mfuasi wa Imam Husein (a.s) aliyemuunga mkono Imamu Husein (a.s) kwenye mapambano ya Karbala, na hatimae kuuwawa katika mapambano hayo, na Ibrahim naye alikuwa ni mfuasi wa Ahlul-Bait (a.s), naye alishiriki katika mapambano yaliyotekea katika vugu vugu la kutaka kulipiza kisasi cha mauaji ya Imam Husein (a.s), vugu vugu ambalo lilianzishwa na Mukhtari Thaqafiy, huku Ibrahim akiwa ni miongoni mwa makamanda wa kivita ndani ya tokeo hilo, yeye aliifanya kazi yake kwa vizuri pasi na woga, na wengi miongoni mwa majahili waliomdhulumu Husein (a.s) walipata jaza yao ya kifo kupitia mkononi mwa Ibrahim, na mmoja miongoni mwa majahili muhimu alioweza kuwateketeza, ni Ibnu Ziad, ambaye alikuwa ndiye shetani mkuu dhidi ya Imamu Husein (a.s). vitabu vya Tarehe vinaelezea kuwa, Ibrahim alikuwa na watoto watano, nao ni: Nuuman, Maalik, Muhammad, Qasim na Khuulaan. Na miongoni mwa watoto hao watano, wapo watoto wawili ambao walikuwa ni wapokezi wa Hadithi, mmoja wao akiwa ni Muhammad na wa pili akiwa ni Qaasim.

JAWABU KWA UFAFANUZI

Maalik bin Harith bin Abdu-Yaghuth bin Salma bin Rabia bin Harith bin Khuzaima bin Sa’ad bin Maalik bin Nukha’a, anatokana na koo mbili asili zilizo shujaa nazo ni Nukha' na Mudh-haj.[1] Yeye alizaliwa katika zama za kijahili kabla ya kuja kwa Uislamu,[2] ama kuhusiana na namna ya kusilimu kwake yeye mwenyewe au ukoo wake, ni moja ya mambo ambayo hayakufafanuliwa na vitabu vya Tarehe, na wala hakuna Hadithi au mfano wa Hadhithi uliolizungumzia suala hilo.[3] Baadhi ya waandishi wanakadiria kuwa yeye alisilimu pale Imamu Ali (a.s) alipokwenda Yemen kuutangaza Uislamu.[4] Kwani makabila mengi yaliukubali Uislamu na kusilimu makundi kwa makundi, kama vile kabila la Hamdaan, Nukha’a na Mudh-haj.

Katika zama za ukhalifa wa Abu Bakar, ukoo huu asili wa Kiarabu ulishika njia ya Sham (Siria) kisha ukaelekea Iraq kwenye mji maarufu ujulikanao kwa jina la (Kuufa), na hapo ndipo yakawa makazi ya kabila hilo, wao walizaliana na kukusanyika siku baada ya siku, hadi ukoo wao ukakua na kuota mizizi ndani ya mji huo. Kizazi cha maalik kilikua siku baada ya siku, na hatimae kizazi hicho kikazaa koo kubwa zilizojulikana kwa jina la (Banu Maalik), (Banu Ibrahim) n.k. Pia hadi leo kuna koo mbali mbali ambazo nasabu zake zinatokana na Maalik Ashtar, na miongoni mwa koo hizo ni Aalu Kaashiful-Ghitaa na Aalu Radhiy.

Imenukuliwa kutoka kwenye vitabu vya Tarehe kuwa, Maalik alikuwa na watoto wawili waliojulikana kwa majina ya Ibrahim na Is-haaq. Is-haaq alikuwa ni mfuasi mkereketwa wa Imamu Husein (a.s) ambaye alishika upanga katika vita vya Karbala baada tu ya kuuwawa kwa Habib bin Madhahir, na hatimae akauwawa katika vita hivyo.[5] Ibrahim alikuwa ni mtoto shujaa wa Maalik Ashtar, ambaye ni mpenzi na mfuasi shupavu wa Ahlul-Bait (a.s). Yeye alikuwa ni Shia madhubuti aliye makini kiimani na kimatendo, na hakufanana tu na baba yake kiimani na kimatendo, bali pia alifanana naye kimwili pamoja na sura.[6] Muandishi maarufu wa Tarehe ajulikanaye kwa umaarufu wa Dhahabiy, amenukuu kutoka kwa waandishi wa Tarehe wa madhehebu ya Kisunni akisema: “Ibrahim alikuwa ni shujaa kama baba yake aliyebobea sifa njema na alikuwa ni miongoni mwa watu watukufu”.[7] Ibrahim alishiriki mapinduzi muhimu yaliosimamishwa na Mukhtari Thaqafiy kwa nia ya kutaka kulipiza kisasi na kuwapandisha katika kiriri cha sheria  wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyengine katika mauwaji ya Imamu Husein (a.s). Ibrahim waliweza kuwatokomeza maadui wengi wa Ahlul-Bait (a.s) ambao walishiriki katika mauaji ya Karbala, na miongoni mwa wale walioteketea kupitia mkononi mwake, ni Ibnu Zaid ambaye alimteketeza ndani ya siku ya kumi ya mwezi wa Muharram ya mwaka 67 Qamaria.[8] Vitabu vya Tarehe vimenukuu kuwa Ibrahim alikuwa na watoto watano waliojulikana kwa majina yafuatayo: Nuumani, Maalik, Muhammad, Qaasim na Khuulaan. Miongoni mwa watoto hawa, mna wale watoto wawili ambao walikuwa ni wapokezi wa Hadithi, nao ni Muhammd na Qaasim.[9]

Kwa ajili ya utafiti zaidi rejea: kitabu (A’ayani Shia) cha Sayyid Muhsin Amin, juz/2, uk/200, Daarut-Ta’ariif lilmatbuua’at, Beirut Lebanon, mwaka 1406 Qamaria.

 


[1] Dairatul-Maarif Shial- A’amma cha  Muhammad Husein A’alamiyul-Haairiy, juz/16, uk/40, chapa ya pili ya Muasastul-A’alamiy lilmatbuua’at, Beirut, chapa ya mwaka 1413. Pia  kitabu A’ayanush-Shia cha Sayyid Muhsin Al-Amin, juz/9, uk/38, chapa ya Dairatul-Ma’arif lilimatbuua’at, Beirut , chapa ya mwaka 1403. Pia kitabu Maalik Ashtar Khutabihi wa Aaraihi, cha Qeisul-Attaar, uk/13, chapa ya kwanza ya Muasasatul-Fikril-Islamiy Iran ya mwaka 1412.

[2] Rejea kitabu Al-A’alaam cha Khairud-Diin Al-Rarkaliy, juz/5, uk/259, chapa ya kwanza ya Daarul-Ilm, Beirut.

[3] Rejea kitabu Maalik Ashtar cha Sayyid Muhammad Ridha Al-Hakim, uk/33, chapa ya kwanza ya Maktabatul-Haidariyya Qum Iran, ya mwaka 1427.

[4] Rejea kitabu Maalik Ashtar cha Muhammad Muhammadiy Ishtihardiy, uk/19, chapa ya pili ya Intishaaraat Peyam Aazaadiy Tehran, mwaka 1372.

[5] Rejea kitabu Maalik Ashtar cha Muhammad Muhammadiy Ishtihardiy, uk/188.

[6] Dairatul-Maarif Shial- A’amma cha  Muhammad Husein A’alamiyul-Haairiy, juz/2, uk/131.

[7] Seiru A’alaamin-Nubalaa cha Dhahabiy, juz/4, uk/35, chapa ya tisa ya Muasasatur-Risaala, Beirut, mwaka 1413.

[8] Rejea kitabu (Al-Kaamil fit-taariikh) imenukuliwa kutoka kwa Ali Munfarid Nadhariy katika kitabu Qissatu Karbala, uk/670, chapa ya sita ya Intishaaraat Suruur, Qum Iran, mwaka 1379.

[9] Rejea gazeti la Risaalat no:6054 la tarhe 16/10/85 Shamsia lililomtafiti Maalik Ashtar na Maisha yake.

 

TARJAMA YA JAWABU KATIKA LUGHA NYENGINE
MAONI
Idadi ya maoni 0
Tafadhali ingiza thamani
mfano : Yourname@YourDomane.ext
Tafadhali ingiza thamani
<< Niburute.
Tafadhali ingiza kiasi sahihi ya usalama Kanuni

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

 • kuna tofauti gani baina ya tabia na eimu ya tabia (saikolojia)?
  22307 Tabia kimtazamo
  Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
 • je hivi mnaweza mkanipatia baadhi ya Riwaya zenye kukataza kuwepo kwa mahusiano baina ya msichana na mvulana?
  8292 Sheria na hukumu
  Msichana na mvulana wanaweza kuwa na aina mbali mbali za mahusiano ndani ya jamii ya wanaadamu, na bila shaka baadhi ya mahusiano hayo huwa si mahusiano salama na si halali. Kwa kweli swali lililo ulizwa na muulizaji wetu, ni swali lisilokuwa la wazi, lakini sisi tutalijibu swali ...
 • Tafadhali naomba munieleweshe, nini maana ya hijja kilugha?
  1212 بیشتر بدانیم
  Hijja kilugha; Ni kukisudia na kukiendea kitu au jambo fulani.[1] Neno hijja Kisheria na kitaalamu; Neno hijja kisheria ni lenye kuashiria aina maalumu ya ibada yenye kutendeka mahala maalumu, kwa mfumo na wakati maalumu. Ibada hii inatakiwa kutendeka katika nyumba maalumu ya Mwenye Ezi ...
 • Niyə müsəlman bir kişi əhli kitab qadını ilə daimi evlənə bilməz amma müvəqqəti evlənə bilər?
  2901 اشتراک در دین
  Kitab əhli qadınları ilə müsəlman kişilərin daimi evliliyi barədə fəqihlərin baxışı müxtəlifdir. Bu ixtilafın səbəbi bu sahədə olan müxtəlif rəvayətlərdən irəli gəlir. Belə nəzərə çarpır ki, bəzi hədislərdə bu evliliyə icazə verlməməsinin hikməti müsəlman kişilərin kafir qadınların əxlaq və xasiyyətlərinin və həmçinin inanclarının təsir altına düşməsinin qarşısını ...
 • ni zipi funga zilizo zisizofaa kwa mtazamo wa imam Shafi, Hanafi na Maalik?
  9277 روزه های مستحب، مکروه و حرام
  Masiku yasiyofaa kufunga saumu mbele ya imam Abu Hanifa ni: siku ya idi ndogo na idi kubwa, pia kufunga siku ya mwezi 11, 12 na 13 ya mwezi wa Dhil-hijja, pia kufunga ndani ya idi pili hadi nne za idi ya mfunguo tatu. Funga zisizofaa ...
 • je kuna haja ya kumkhofu Mola au tunatakiwa kuwa na mapenzi Naye?
  5512 محبت و دوستی
  Suala la mtu kuwa na khofu huku akiwa na matarajio ya kheri, na kwa upande wa pili akawa na mapenzi ya Mola wake, huwa si suala la kushangaza, kwa mambo hayo mawili hayapingani katika kuwepo kwake, kwani kuwepo kwa hali mbili kama hizo huwa ni jambo la ...
 • nini maana ya ucha Mungu?
  11555 تقوی
  Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
 • nini maana ya neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر) lililonasibishwa na Mungu ndani ya Qur-ani?
  12130 مکر
  Neno (kupanga mipango ambalo kwa Kiarabu ni مکر), humaanisha utafutaji wa hila au njia katika kulifikia jambo fulani, na yawezekana mtu kutafuta hila na njia za kuyafikia mazuri au mabaya. Ujanja wa Mungu: kuna Aya tofauti ambazo zimeliegemeza na kulinasibisha neno (ujanja مکر) ...
 • nini ilikuwa hatima ya farasi wa Imamu Husein (a.s) huko Karbala?
  4529 حوادث روز عاشورا
  Waandishi mbali mbali wa walioandika na kulizungumzia tokeo la Karbala, hawakutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na farasi wa Imamu Husein (a.s), bali walichokielezea ni kuwa, farasi huyu alijipakaa damu ya Imamu Husein (a.s), kisha akaelekea kwenye mahema huku akitoa sauti kali yenye kuashiria huzuni na hasira. Watu ...
 • hivi mvuta sigara aweza kuvuta sigara hali akiwa amefunga?
  3948 رساندن دود و غبار غلیظ به حلق
  Wanazuoni wote wa Kifiqhi wanasema kuwa: ni wajibu wa kila mwenye funga kuchukuwa tahadhari, na kutofikisha kitu chochote kile kama vile tumbaku au moshi wa sigara ndani ya koo yake.[1] Na hakuna hata mmoja miongoni mwa wanazuoni aliyetoa ruhusa ya kuvuta sigara ...

YALIYOSOMWA ZAIDI