advanced Search

Uislamu ni dini ya matendo, na malipo ya matendo hayo yapo kwa Mola mwnyewe, na ujira bora zaidi juu ya matendo hayo humuangukia yule mwenye matendo yaliotimia zaida kiikhlasi, na Mola ndiye mlipaji bora kuliko walipaji wote, naye hatoupoteza ujiwa wa mtu yoyote yule miongoni mwa watendaji hao.[1] Kila nia ya mja juu ya matendo ayatendayo inapokamilika kiikhlasi, na kila mja apostahamili madhila na mitihani mbali mbali kwa ajili ya Mola wake, ndipo anapopata ujira mkubwa zaidi, na thamani yake huwa ni kubwa zaidi mbele ya Mola wake. Na msingi huo ndio uliowafanya mitume na Maimamu (a.s) kuwa na cheo kikubwa zaidi kuliko wengine mbele ya Mola wao. Imamu Husein naye (a.s) ambaye ni Imamu wa tatu wa Kishia, ni mtu mwenye cheo kikubwa mbele ya Mola wake.

Cheo chake hicho hakukipata kwa sababu ya nasaba yake ambayo ni nasaba iliyoungana moja kwa moja na Mtume (a.s.w.w), bali cheo hicho amekipata kw kutokana na makusudio ya malengo aliokuwa nayo, matendo yaliyokamilika, mitihani mbali mbali pamoja na kukubali jukumu la kujitoa muhanga kwa ajili ya kuinusuru dini ya Mola wake. Yeye (a.s) pale alipokabiliana na Yazidu katika mapambano ya Karbala, hakuwa na malengo ya kidunia yaliyotokana na nafsi yake, bali malengo yake yalikuwa ni kuiokoa dini ya Mola wake, pamoja na kuirejeshea dini hiyo heshima yake iliokuwa tayari imeshaanza kupotezwa. Leo imekuwa ni jambo la wazi ka kila mwenye akili timamu kuwa, iwapo Imamu Husein (a.s) hangesimama kidete mbele ya utawala wa Banii-Umayya, basi sisi leo tungelibakiwa na jina tu la Uislamu. Leo uhakika wa dini ungelibakia kuwa ni mateka wa Banii-Umayya, na wala uhakika wa Uislamu usingeweza kutufikia sisi tunaoishi katika zama hizi. Kujitoa kwake muhanga Imamu Husein (a.s), ulikuwa ni mchanganyiko wa mapenzi na akili iliyotimia, mchanganyiko ambao uliweza kufanya kazi kisawasawa hadi kuuangusha utawala wa kidhalimu wa Banii-Umayya. Na kwa upande wa pili Imamu Husein (a.s), alielewa wazi kuwa Yeye (a.s) hana hata njia moja itakayomuwezesha kuishi, kwani Yeye (a.s) alielewa wazi kuwa lengo la Yazidu ni kumuondoa Yeye (a.s) duniani, pia alielewa namna ya unafiki wa watu wa mji wa (Kuufa) ulivyokomaa, kwani unafiki wao ulikwisha mdhihirikia yeye pale wao walipouonesha unafiki wao kwa Ali bin Abii-Taali na kwa Hassan bin Ali (a..s). Pamoja na yote hayo, lakini yeye hakurudi nyuma, bali aliikusanya familia yake na kuelea vitani bila ya khofu wala woga, naye alipigana vita hivyo kwa moyo wa ukunjufu mbele ya Mola wake, na mwishowe damu yake takatifu ikama ndiyo mbolea iliyouimarisha Uislamu na kuutoa katika unyonge.

 

Ingawaje kuna wengi waliouza roho zao kwa ajili ya Mola wao, lakini hakuna hata vita vimoja vilivyoweza kulingana na tokeo la Mauwaji ya Karbala, kwani hakukutokea mauwaji ya kikatila zaidi ya mauwaji hayo! Mola mtukufu katika Qur-ani anasema: “Kwa hakika Sisi tunawalipa wenye kusubiri ujira wao bila ya hesabu”![2] je Tarehe imeweza kunukuu kisa chenye mauwaji ya kigaidi zaidi ya mauwaji ya Karbala? Na je kuna mtu aliyekuwa na subra zaidi ya Imamu Husein (a.s)? Subra yake na kujitoa kwake muhanga, hakukuwa na na hata chembe moja ya kutafuta maslahi binafsi. Ni ujira gani basi utokao kwa Mola, anaostahiki mtu kama huyo kuupata.

Mwenye Ezi Mungu amempa Yeye (a.s) ujira na utukufu usio na kifani, miongoni mwa fadhila na utukuffu aliopewa na Mola wake, ni kule kuhimizwa watu kulizuru kaburi lake, huku watu hao wakiahidiwa fadhila kubwa kutoka kwa mola wao kwa yule atakayemzuru Imamu Husein (a.s). moja kati ya  Hadithi zilizowaahidi watu watakaomzuru Yeye (a.s) kupata fadhila kubwa, ni ile Hadithi Mutawaatiru iliyonukuliwa na Shekh Mufiid, Hadithi hiyo ni kama ifuatavyo: Imamu Jaafar Saadiq (a.s) amesema: ““…Na mtu atakayelizuru kaburi la Imamu Husein siku ya Ashura, fadhila zake ni kana kwamba mtu huyo amekutana na Mola wake katika Arshi ya Mwenye Ezi Mungu”.[3] Na wala hakuna jambo la ajabu kuhusiana na Hadithi hii, Kwani kuna Hadithi nyingi zenye kuzungumzia aina kama hiyo ya fadhila kwa yule atakayemzuru Mtume (s.a.w.w), na  Hadithi hii inayozungumzia fadhila hizi, inafanana na ile Hadithi ya Imamu Ridha (a.s), inayozungumzia fadhila za kulizuru kaburi la Mtume (s.a.w.w), na Hadithi hiyo ni kama ifuatavyo: Imamu Ridha (a.s) alipokuwa akiwafahamisha watu maana ya kumzuru Mola alisema: “Kwa kutokana kwamba, kumuona na kumzuru Mola ni jambo lisilowezekana, hivyo basi Mola mwenyewe amejaalia kuwa, kumzuru Mtume wake (s.a.w.w) ni sawa na kumzuru Yeye (s.a)”.[4]

 

Lakini hapa tunatakiwa kuwa na mazingatio ya kwamba, kumzuru Imamu Husein (a.s), ni moja kati ya sababu zinazosababisha kudumu na kubakia hai malengo ya Imamu Husein (a.s), na kubakia hai huko kwa malengo hayo, ni sawa na kubakia hai kwa dini ya Mola, jambo ambalo limetiliwa mkazo na ibara mbali mbali za Qur-ani tukufu.

 

 


[1] Suratu Aalu-Imraan Aya ya 171. Suratut-Tawba Aya ya 120.

[2] Suratuz-Zumar Aya 10.

[3] Na maandiko ya Hadithi hiyo ni kama ifuatavyo:

-  جَعْفَرُ بْنُ مُحَمَّدِ بْنِ قُولَوَيْهِ فِي الْمَزَارِ عَنْ جَعْفَرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْمُوسَوِيِّ عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ نَهِيكٍ عَنِ ابْنِ أَبِي عُمَيْرٍ عَنْ زَيْدٍ الشَّحَّامِ عَنْ جَعْفَرِ بْنِ مُحَمَّدٍ ع قَالَ مَنْ زَارَ الْحُسَيْنَ ع لَيْلَةَ النِّصْفِ مِنْ شَعْبَانَ غَفَرَ اللَّهُ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ وَ مَا تَأَخَّرَ وَ مَنْ زَارَهُ يَوْمَ عَرَفَةَ كَتَبَ اللَّهُ لَهُ أَلْفَ حَجَّةٍ مُتَقَبَّلَةٍ وَ أَلْفَ عُمْرَةٍ مَبْرُورَةٍ وَ مَنْ زَارَهُ يَوْمَ عَاشُورَاءَ فَكَأَنَّمَا زَارَ اللَّهَ فَوْقَ عَرْشِهِ.

[4] Rejea kitabu (Tah-dhiibul-Ah-kaam), juz/6, uk/3. Na maandiko ya Hadithi hiyo ni kama iffuatavyo:

قاْلِ الصَّادِقِ ع مَنْ زَارَ رَسُولَ اللَّهِ ص كَمَنْ زَارَ اللَّهَ فَوْقَ عَرْشِهِ ؛ وسائل‏الشيعة ج : 14 ص : 335،حدیث 19340، وَ عَنْ عِدَّةٍ مِنْ أَصْحَابِنَا عَنْ سَهْلِ بْنِ زِيَادٍ عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ الْحُسَيْنِ عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْمَاعِيلَ عَنْ صَالِحِ بْنِ عُقْبَةَ عَنْ زَيْدٍ الشَّحَّامِ قَالَ قُلْتُ لِأَبِي عَبْدِ اللَّهِ ع مَا لِمَنْ زَارَ رَسُولَ اللَّهِ ص قَالَ كَمَنْ زَارَ اللَّهَ فَوْقَ عَرْشِهِ الْحَدِيثَ.

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

  • kuna njia gani za kujenga urafiki na Qur-ani zitakazo mfanya mtu azoeane na Qur-ani?
    13887 Tabia kimatendo 2012/05/23
    Kama mtu atakaye isoma Qur-ani kwa nia ya kutafuta radhi za Mola wake, huku yeye akawa anaisoma Qur-ani hiyo kwa makini na kuitafakari vilivyo, basi Qur-ani iatamvuta mtu huyo na kumfanya awe ni mpezi wake wa rohoni. ...
  • nini maana ya ucha Mungu?
    22047 تقوی 2012/05/23
    Taqwa (ucha Mungu) ni nguvu maalumu za kiroho zinazo weza kupatikana ndani ya nafsi ya mwanaadamu, nguvu ambazo huwa ni himaya maalumu inayomuwezesha yeye kujitenga na maasi. Taqwa kamili ni ile inayomfanya mtu kujiepusha na maasi yanayo eleweka na kila mmoja wetu, pamoja na kujiepusha na yale ...
  • kwa nini Imamu Husein (a.s) anaitwa Tharu-Llahi (ثار الله)?
    13034 زیارت عاشورا و دیگر زیارات 2012/05/23
    Neno Tharu-Llahi (ثار الله) limekuja likiwa na maana mbili: moja ni kwa maana ya damu, na ya pili ni kwa maana ya kulipiza kisasi na kutaka kummwga damu ya muuwaji. Kwa hiyo maana ya mwanzo inapotumika kwa ajili ya kumuita Yeye (a.s) Tharu-Llahi (
  • Nini maana ya Feminism?
    17340 Sheria na hukumu 2012/05/23
    Neno (Feminism) linatokana na lugha ya Kifaransa ambalo asili yake ya Kilatini ni (Femind), neno hili hutumika katika lugha mbali mbali huku likiwa na maana moja inayomaanisha uke au jinsia ya kike, ijapokuwa neno hili linapotumika kutoka lugha moja kwenda nyengine huonekana kuwa na mabadiliko kidogo ya ...
  • kuna tofauti gani baina ya tabia na eimu ya tabia (saikolojia)?
    33689 Tabia kimtazamo 2012/06/17
    Neno (tabia) linatokana na neno la Kiarabu (اخلاق) ambalo ni umoja wa neno (خُلْق) lenye maana ya tabia, nyenendo au sifa za watu mbali mbali zinazo zimbatana na matendo yao bila ya kutofautisha baina ya sifa na tabia mbaya na zile sifa njema.
  • nini hukumu ya msafiri aliyefunga, ambaye atasafiri kabla au baada ya kuingia Adhuhuri?
    9376 گوناگون 2012/05/23
    1- safari itakayo fanywa baada ya adhuhuri huwa haiharibu funga, na funga ya siku hiyo itakuwa sahihi.[1] 2- na mtu ambaye yuko safarini kisha akaamua kurudi kwake kabla ya adhuhuri, au akaamua kwenda sehemu ambayo ana nia ya kuweka makazi yake hapo ...
  • je kuna haja ya kumkhofu Mola au tunatakiwa kuwa na mapenzi Naye?
    10771 محبت و دوستی 2012/05/23
    Suala la mtu kuwa na khofu huku akiwa na matarajio ya kheri, na kwa upande wa pili akawa na mapenzi ya Mola wake, huwa si suala la kushangaza, kwa mambo hayo mawili hayapingani katika kuwepo kwake, kwani kuwepo kwa hali mbili kama hizo huwa ni jambo la ...
  • Shin aure yana da wasu sharaDai na musamman?.
    7477 Sheria na hukumu 2017/05/22
    A mahangar musulunci auren da’imi da na mutu’a suna da sharaDai waDanda sune kamar haka:- 1. Karanto siga (Yarjewa juna tsakanin miji da mata shi kaDai bai wadatar ba lalle ne a hada shi da furta “farar da” lafazi na musamman). 2. Bisa ihtiyaDi na wajibi ya ...
  • nini hukumu ya kufuga njiwa ndani ya sheria za Kiislamu? Na nini msingi hasa wa hukumu hiyo?
    26483 نگهداری و شکار حیوانات 2012/06/17
    Tukilitazama suala la kufunga njiwa kibinafsi, tutalikutia kuwa suala hili halina matatizo na ni halali. Lakini pale sisi tutapolimbatanisha suala hili na haki za majirani au wanajamii, hapo tunaweza kulipa picha ya uhalali au uharamu kwa jinsi hali za jamii mbali mbali zinavyolitazama suala hilo. Baadhi ya ...
  • hivi Abbaaasi alipokwenda mto Furaat kwa ajili ya kuwaletea maji watu wa familia ya Imamu Husein (a.s) alitumia utajo au ukulele maalumu?
    8512 اهل بیت و یاران 2012/05/23
    Imamu Husein (a.s) pamoja na wafuasi wake pale walipokuwa Karbala, walikuwa wakisoma mashairi maalumu yenye ibara za kivita, kwa ajili ya kuwahamasisha wanavita, pia Abul-Fadhlil-Abbaas alionekana mara zote katika siku ya Ashura kusoma aina mbali mbali za ibara na mashairi ya kuvutia kwa ajili ya uhamasishaji, mashairi ...

YALIYOSOMWA ZAIDI