advanced Search

Kwa mujibu wa nukuu za baadhi ya Hadithi ni kwamba, majina ya matano ya Aali Abaa (a.s), yaani Aali wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambao ni: Ali, Fatima,Hasan na Husein, yametajwa ndani ya Taurati na Injili. Pia suala hilo linaonekana kuashiriwa ndani ya ile Hadithi yenye kunukuu majadilianao ya kielimu yalipita baina ya Imamu Ridha (a.s) na watu wawili, ambao ni Jaaliith ambaye ni miongoni mwa viongozi wa Kanisa, na Ra-asul-Jaaluut ambaye ni miongoni mwa wakuu wa Kiyahudi.

Ingawaje yawezekana upotoshwaji uliopatikana ndani ya Taurati na Injili ilioko mikononi mwa waumini wa Kikristo, ukawa umeyafuta majina ya watukufu hao, [1] lakini bado kuna Hadithi zenye kuelezea kuwa majina hayo yalikuwa ni maarufu ndani ya vitabu hivyo, nao walikuwa wakijulikana kwa jina la Aalu Abaa (a.s), na ibara hii ilikuwa ikiwakusudia: Mtume Muhammad (s.a.w.w), Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s), pia suala la majina ya watukufu hao (a.s) kuwemo ndani ya Injili na Taurati, ni lenye kuonekana ndani ya Hadithi yenye kuyanukuu majadilianao ya kielimu yaliopita baina ya Imamu Ridha (a.s) na watu wawili, ambo ni Jaaliith aliyekuwa ni miongoni mwa viongozi wa Kanisa, na Ra-asul-Jaaluut ambaye ni miongoni mwa wakuu wa Kiyahudi. Imamu Ridha (a.s) katika majadiliano yake na watu hao, alisimama kidete na kutumia dalili mbali mbali zenye kukinaisha, huku Yeye (a.s) akimuambia Jaalithi: “Amini basi (kama kweli unataka kuifuata haki na njia ilionyooka)” hapo Jaalith alimuelekea Imamu (a.s), kisha akamuambia: “huyu Mtume unayemtaja na kutaka kuuthibitisha utume wake, ametajwa ndani ya Taurati na Injili! Na utume wake umebashiriwa ndani ya vitabu hivyo, jina lake ni Muhammad (s.a.w.w), na wasii wake ni Ali, na bint yake ni Fatima na wanawe (wajukuu zake) ni Hasan na Husein…” pia Imamu (a.s) ndani ya majadiliano haya, alionekana kumkabili Ra-asul-Jaaluut kwa dalili mbali mbali kutoka ndani ya Taurati. Baada ya majadiliano ya muda mrefu Ra-asul-Jaaluut alisema: “kwa kweli kizingiti kikubwa mbele yangu katika kuukubali ukweli huu, ni uluwa na ukubwa niliopewa na Mayahudi, na kama hali isingekuwa hiyo, basi mimi ningelisilimu, kwa kweli mimi sijapata kumuona mtu mjuzi zaidi wa Taurati na Injili kuliko wewe. Kwa kweli ndani ya Taurati kumetajwa majina ya watu hawa, ambao ndani ya Taurati yetu, Mtume huyu ametajwa kwa jina la Ahmaad na Ilyaa, kisha akatajwa bint yake, pia ndani yake wametajwa Shubbar na Shubeir, ambao kwa Kiarabu ni Muhammad (s.a.w.w), Ali, Fatima, na Hasana na Husein…”[2]  Kipengele hichi cha Hadithi ni chenye kutoa muangaza wa kutosha kuhusiana na kukiri kwa  wakuu wa Kiyahudi na  Kikristo juu ya kutajwa kwa majina ya wale watu watano watukufu ndani ya Taurati na Injili.

 


[1] Katika tafiti zetu mbali mbali za kujibu maswali ya hapa na pale, tayari suala hili la upotoshwaji wa Taurati na Injili tumeshalitafiti, kwa hiyo iwapo kutahitajika dalili au mada kuhusu hilo, unaweza kurudia kwenye kipengele husika ndani ya jawabu na tafiti zetu mbali mbali.

[2] Biharul-anwaar, juz/49, uk76 hadi 78, mlango wa 4.

MPANGILIO WA KIMAUDHUI

MASWALI KIHOLELA

YALIYOSOMWA ZAIDI